EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, May 28, 2015

WANANCHI WATAKIWA KUTOA TAARIFA ZA UKIUKAJI WA KANUNI NA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

Naibu kamishna wa jeshi la polisi kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Johanes Kahatano (katikati) akiwafafanulia jambo Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kushoto), Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamishna Msaidizi wa Polisi Mohamed Mpinga, na Mkurugenzi wa Radio One Stereo, Deogratius Rweyunga kuhusiana na  kampeni ya kuzuia ajali barabarani inayojulikana kama “Zuia Ajali Sasa, Toa Taarifa Mapema”  kupitia namba 0800757575. Kampeni inayoendeshwa na jeshi la polisi  kikosi cha Usalama barabarani, Vodacom Tanzania na vyombo vya habari vya kampuni ya IPP .
Mkuu wa jeshi la polisi kikosi cha Usalama Barabarani, Kamanda Mohamed Mpinga (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kushoto) kuhusiana na kampeni hiyo.
Deogratius Rweyunga (katikati) akibandika stika yenye namba 0800757575 ambayo imetolewa mahsusi kwa abiria wanaotumia vyombo vya moto kusafiria ili kutoa taarifa bure kuhusu ukiukaji wa sheria na kanuni za usalama barabarani kupitia namba hizo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Zuia Ajali Sasa, Toa Taarifa Mapema”.



Ni kupitia kampeni ya Zuia ajali sasa,toa taarifa mapema

Dar es Salaam, Mei 27, 2015: Kufuatia wimbi la ajali lililosababisha vifo vya mamia ya watu na maelfu wengine kujeruhiwa, wananchi wametakiwa kuunga mkono jitihada za kupunguza ajali nchini kwa kutoa taarifa kwa vyombo ya usalama waonapo kanuni na sheria za barabarani zinakiukwa na madereva wazembe hasa wanapokuwa wanasafiri na magari yaendayo masafa marefu.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamishna Msaidizi wa Polisi Mohamed Mpinga wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya kuhamasisha usalama barabarani ijulikanayo kama “Zuia Ajali Sasa,Toa Taarifa Mapema”  inayofanyika kwa ushirikiano wa serikali kupitia Jeshi la Polisi, kampuni ya mawasiliano ya Vodacom na kampuni ya vyombo vya habari vya IPP. Uzinduzi huo umeambatana na kuzinduliwa na namba maalumu ya kutoa taarifa za ukiukwaji wa kanuni na usalama barabarani ambayo ni: 0800757575.
“Matukio ya ajali hapa nchini yatapungua iwapo watumaji wa barabara hususan madereva watazingatia sheria na kanuni za usalama baabarani na ni jukumu letu sote kuvalia njuga tatizo hili  na kutoa taarifa za madereva na watumiaji wa  barabara wazembe kwa vyombo vinavyohusika ili wachukuliwe hatua za kisheria. Nayapongeza makampuni ya Vodacom na IPP Media kwa kuungana na Jeshi la Polisi katika kampeni hizi,” alisema Kamanda Mpinga.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Mkuu wa Mawasiliano ya makampuni na Uhusiano wa Vodacom Rosalynn Mworia amesema “Tukiwa kampuni ya mawasiliano tutaendelea kuunga mkono jitihada za kupunguza ajali nchini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walioko katika mapambano haya. Leo tumetoa namba ya simu ya kutoa taarifa za ukiukwaji wa sheria barabarani ambayo ni ya bure kwa wateja wa Vodacom. Mteja atakayepiga kutoa taarifa kupitia namba hii hatatozwa gharama zozote bali tutazibeba ikiwa moja ya jitihada za kuunga mkono kampeni hizi. Nawakumbusha watumiaji wa barabara tuzingatie sheria na kanuni na tusisite kutoa taarifa kwa vyombo husika tunapoona vitendo vya kuhatarisha maisha kutoka kwa watumiaji wa barabara wazembe,” alisema.
Vodacom imekuwa mstari wa mbele katika kampeni za uhamasishaji usalama barabarani na mwaka jana ilizindua kampeni ya “Wait to Send” inayohamasisha madereva kutotumia simu za mkononi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto na kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani.
Wakati wa uzinduzi wa kampeni hii uliofanyika katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha  Ubungo ambapo madereva waligawiwa pete maalumu za kuwakumbusha kuacha matumizi ya simu wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto, pia waligawiwa vipeperushi ya kuwakumbusha kanuni na sheria za usalama barabarani. Pia abiria walihimizwa kutoa taarifa za uzembe wa madereva wanapokuwa safarini kupita vibandiko vyenye ujumbe wa kampeni hii usemao “Zuia Ajali Sasa,Toa Taarifa Mapema” vyenye namba ya kutoa taarifa ya: 0800757575..
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Radio One Stereo, Deogratius Rweyunga alisema kuwa kampeni hii muhimu ina uwezo wa kupunguza kwa kiasi kikubwa nap engine kutokomeza kabisa kupitia teknolojia za mawasiliano.
“Kampeni tunayoizindua leo itahusisha kurushwa kwa taarifa na matukio ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani kupitia Radio One Stereo, ITV na Capital Radio. Kusudi kubwa la kufanya hivi ni kuendeleza ujumbe wa usalama barabarani ka upana zaidi na pia kuwaweka bayana wale wote wanaokiuka na kuvunja sheria za usalama barabarani kwa makusudi kabisa. Tutatumia pia uwepo wetu katika mtandao kupitia Twitter na Facebook katika kuhakikisha tunatumia kila nafasi kusambaza ujumbe huu muhimu,” alisema Rweyunga.
Aliongeza kuwa ushirikiano kati ya vyombo vyao vya habari na Vodacom Tanzania utafanikiwa na kuchangia kwa kiasi kikubwa kampeni hii ya uhamasishaji wa umma. Kujitolea kwa vyombo hivi vya habari kutaisaidia kampeni hii kufikia malengo yake yote, kubwa haswa likiwa kufanya barabara kuwa njia salama kuliko zote za usafiri.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate