EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, October 31, 2014

MSIBA: MTANGAZAJI BEN KIKO AFARIKI DUNIA



Ben Kiko enzi za uhai wake.
ALIYEKUWA mtangazaji maarufu wa Radio Tanzania, Ben Kiko, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Oktoba 31, 2014 akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa akitibiwa.
Kiko amefariki baada ya kusumbuliwa na maradhi ya figo kwa muda mrefu.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN.

WEMA AMMWAGA DIAMOND!


Na Musa mateja
Safari hii ndiyo basi tena! Pamoja na kujishaua mbele ya kamera za wanahabari na simu za kuteleza (smart phones) kisha kutupia kwenye mitandao ya kijamii wakizuga wapo pamoja, habari ya mjini inadai kwamba, sexy lady wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ amemmwaga staa wa Ngoma ya Mdogomdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Sexy lady wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’.
KUMBE NI MUDA MREFU TU
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni rafiki mkubwa wa wapenzi hao, ishu ya kumwagana ilikuwepo muda mrefu lakini kinachoendelea ni kuwazuga mashabiki wao ili wasishuke kisanaa.

BINTI DARASA LA TANO ATUNDIKWA MIMBA NA DENTI MWENZAKE


CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
Mtoto mmoja aliyejulikana kwa jina la Paulina (14) mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Boko, jijini Dar amekatisha masomo kutokana na kupata ujauzito.
Mtoto anayejulikana kwa jina la Paulina (14) alitundikwa mimba na mawanafunzi mwenzake.
Akizungumza kwa huzuni huku akilia, mtoto huyo alisema kwa sasa haendi shuleni kutokana na kuwa na ujauzito wa miezi miwili alioupata kwa kijana aliyemtaja kwa jina moja la Paulo mkazi wa Mbweni ambaye ni mwanafunzi wa sekondari. Alisema:
“Paulo alikuwa rafiki wa kaka yangu na alikuwa akija sana nyumbani kwetu, tukawa tumezoeana sana na siku moja akanishawishi twende kwao, tukaenda na huko ndiyo tukafanya mapenzi baada ya kuniambia atanioa nikimaliza shule.

FUMANIZI LA AINA YAKE


MAKONGORO OGING’ NA HARUNI SANCHAWA
HILI ni fumanizi la aina yake! Achana na mafumanizi ya kawaida ambayo yamezoeleka, la safari hii ni la kipekee baada ya mgoni aitwaye Kibole Kalepe kukutwa chumbani na mke wa mtu, Asha Hemedi (pichani) kisha kukurupuka na kupanda darini haraka kukwepa kipigo, Ijumaa lina mkasa kamili.
Mbaba Kibole Kalepe akiwa darini kuepusha kipigo baada ya fumanizi.
Tukio hilo lililofunga umati wa watu wapenda ubuyu lilijiri Oktoba 28, mwaka huu maeneo ya Iteba-Sinza, jijini Dar baada ya mwenye mali, aitwaye Fikiri kurejea ghafla nyumbani na kumkuta mkewe akiwa chumbani na Kibole wakifanya yao.

MADAHA ATILIA SHAKA AFYA YA ‘MKONGO WA WOLPER’


Msanii wa filamu na muziki, Baby Joseph Madaha amesema ana wasiwasi na afya ya mwanaume Mkongo anayefahamika kwa jina la Mwani aliyewahi kuwa mpenzi wa Jacqueline Wolper.
Msanii wa filamu na muziki, Baby Joseph Madaha
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Baby Madaha alisema, hofu yake hiyo inatokana na namna mwanaume huyo anavyotapanya pesa huku akitangaza dau kubwa ili kuwapata mastaa wa kike.

Thursday, October 30, 2014

TIM COOK WA KAMPUNI YA APPLE ASEMA ANA FAHARI KUWA SHOGA



Mtendaji Mkuu wa Apple, Tim Cook.
MTENDAJI Mkuu wa kampuni ya Apple ya Marekani, Tim Cook, amefichua kwamba yeye ni shoga na anaona fahari kuwa hivyo.

Cook ameyasema hayo leo katika tahariri ya mtandao wa Businessweek.com kwamba: “Acha niseme wazi. Ninaona fahari kuwa shoga, na ninaona kuwa shoga ni moja ya zawadi kubwa zaidi ambazo Mungu amenipa.”
Ameongeza kusema kwamba wafanyakazi “wengi” wa Apple wanafahamu kwamba yeye ni shoga na haoni tofauti yoyote kuhusu wanavyoshirikiana naye.
Cook anakiri kwamba jambo la kufichua hali hiyo halikuwa rahisi, lakini alifanya hivyo kwa kutaka jamii imwone yuko sawa na watu wengine.
“Sijioni kuwa mwanaharakati katika jambo hili, bali ninatambua nilivyonufaika katika kujitoa mhanga kwa wengine.

MSIBA : Muigizaji Mzee Manento amefariki dunia

MSIBA : Muigizaji Mzee Manento amefariki dunia.
Habari zilizotufukia hivi punde zinasema kuwa muigizaji Mzee Manento amefariki dunia hapo jana. Bado tunafuatilia kwa karibu habari hizi nz chanzo ch kifo cha mzee wetu huyu.
Mzee Mnento atakumbukwa hasa kwa filamu alizocheza kiumakin na marehemu Kanumba. Hero of the church, Dar to lagos,fake pastor n.k pumzika kwa Amani
Mungu ailaze Roho ya maerehemu mahali pema peponi amina.

WAZIRI WA FEDHA SAADA MKUYA AZINDUZI WA CHAPISHO KUU LA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI YA KAYA BINAFSI 2011-2012-TANZANIA BARA‏


Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum (Katikati) akionyesha kitabu cha Ripoti ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa Mwaka 2011/12 wakati akikizindua katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam jana Oktoba 29, 2014. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Ofisa kutoka Shirika la Maendeleo la DPG, Sinikka Antila, Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Philippe Dongier na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu.  Picha/Video zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha Ripoti ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa Mwaka 2011/12 wakati akikizindua katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam jana Oktoba 29, 2014. Wanaoshuhudia ni Afisa Habari wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Veronika Kazimoto (kulia) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu (katikati).

NI SHEEDAH 'WEMA, AUNTY HUSAGANA'

Stori: Musa Mateja na Imelda Mtema
Ni sheedah! Pamoja na kukanusha kwa kutumia nguvu kubwa, nyuma ya ushosti wa mastaa grade one wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na Aunty Ezekiel kuna siri nzito ikidaiwa kwamba wawili hao husagana.Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na Aunty Ezekiel wakidendeka hadhalani.
TUKIO BICHI
Madai hayo ya muda mrefu huku wenyewe wakisisitiza si ya kweli, yameibuka upya juzikati baada ya warembo hao kuonesha mahaba niue au nikongorowe kisha ‘kudendeka’ hadharani na kusababisha mwandani wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kukasirika na kuondoka eneo la tukio akiambatana na timu yake ya Wasafi Classic Baby (WCB).

CHEKI MSIMBAZI WALIVYOZIKARABATI OFISI ZAO ZA MSIMBAZI SASA NI KAMILI

PICHA ZOTE NA SALEH JEMBE.COM
OFISI ZA MAKAO MAKUU BAADA YA KUKARABATIWA...TASWIRA MPYA

SIYO DHAMBI KUMPENDA MPENZI WA MWENZAKO ILA FANYA HIVI…

Utafiti ambao umefanyika unaonesha kuwa, asilimia kubwa wapo kwenye uhusiano na watu ambao siyo waliopangiwa na Mungu kuwa nao.Kutokana na hilo ndiyo maana utakubaliana na mimi kwamba, usaliti umekuwa ukishamiri, watu wamekuwa wakiachana kila siku na wengine kuendelea kuishi pamoja lakini si kwa amani.
Hii ni kwa sababu wameingia kwenye penzi na watu ambao si sahihi. Kutokana na mazingira hayo, haiwezi kuwa kitu cha ajabu mume wa mtu kutokea kumpenda sana mke wa mtu au kinyume chake.
Pia huwezi kuonekana mwendawazimu kwa kumpenda mtu ambaye tayari ana mpenzi wake. Hii ni kwa sababu inawezekana una mapenzi ya kweli zaidi kwake kuliko huyo aliye naye. Hata hivyo, hakuna kitu kibaya kama kuanzisha uhusiano na mtu ambaye tayari ana mpenzi wake au ameshaingia kwenye ndoa. Utakuwa unatafuta matatizo kama utamtongoza mke wa mtu au utaonesha kumzimikia mume wa mtu na kujikuta ukishawishika kutaka kumpasulia ukweli.

ROSE NDAUKA: SIFAGILII WANAUME TENA

Stori: Mayasa Mariwata
STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka amesema kuwa kwa sasa yupo bize na malezi ya mwanaye hivyo hana mpango wa kuwa na mwanaume yeyote hata awe pedeshee mwenye uwezo wa fedha kiasi gani kwani mwenyewe anajitosheleza.
Staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka.
Akipiga stori na paparazi wetu alisema, kipindi hiki hafagilii kabisa mambo ya mabwana na wala hahitaji mapedeshee kwa kuwa yeye mwenyewe ana uwezo wa kujitosheleza kifedha. “Mimi sina bwana kwa sasa na wala sihitaji hao mapedeshee, watanisaidia nini wakati nafanya kazi zangu zinazoweza kuniingizia fedha, nina akili timamu, nina miguu na nina macho sasa kwa nini nitegemee pesa ya mtu?” alihoji Rose.
Kwa mara ya kwanza...

Wednesday, October 29, 2014

Ajali mbaya yaua eneo la Tengeru, Arusha

Imetokea ajali mbaya eneo la Tengeru kuelekea Usa, kati ya lory na gari dogo la abiria (hiace) watu kadha wamefariki na majeruhi ni wengi.
Picha ndio hizo hapo.
Watu 9 wamekufa na wengine 2 wamejeruhiwa baada ya basi dogo la abiria Toyota Hiace kugongana uso kwa uso na lori mafuta katika eneo la Usa River, Arusha

Source; RADIO ONE STEREO

ABIRIA WA BUKOBA WALALAMIKIA BASI LA MOHAMMED TRANS


Muonekano wa basi hilo.
ABIRIA waliokuwa wakisafiri na basi la Kampuni ya Mohammed Trans leo lenye namba za usajili T 774 AWJ kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Bukoba wamelalamikia basi hilo kuwa ni bovu.

Sehemu ya mlango wa abiria.

TRENI LA MIZIGO LAPATA AJALI DAR


Treni la mizigo baada ya kupata ajali.
TRENI la mizigo limepata ajali eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam muda mfupi uliopita na kuangusha mabehewa yaliyokuwa na makontena ya Azam na Mohamed Enterprises.

Makontena yaliyokuwa yamebebwa na treni hilo la mizigo.
Kikosi cha Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU) tayari kimefika eneo la tukio kuimarisha ulinzi wa mali zilizokuwemo katika mabehewa hayo.

ROSE MUHANDO ADAIWA KUBWIA UNGA!

Stori: Mwandishi Wetu HUKU mwenyewe akikanusha vikali kwamba hatumii, nyota wa muziki wa Injili Bongo, Rose Muhando bado anaandamwa na madai mazito kwamba anatumia madawa ya kulevya ‘unga’ yanayomfanya kuwa hoi kiasi cha kushindwa kutokea kwenye matamasha mbalimbali anayolipwa fedha, Risasi Jumatano linateremka nayo.
Nyota wa muziki wa Injili Bongo, Rose Muhando.
Kwa mujibu wa vyanzo, Rose anadaiwa kutumia unga kiasi kwamba, baada ya matumizi hujikuta akishindwa kufanya jambo lolote lile la kujitafutia mkate wake wa kila siku na ndiyo maana amekuwa akikwaa skendo za kupokea fedha za shoo halafu hatokei tu!
WATOA MADAI
Hivi karibuni, akina mama watatu walifika kwenye Ofisi za Global Publisheers na kumtolea madai Rose kuhusu tuhuma zanazomwandama kwamba amekuwa akiingia mitini na fedha za watu wanaomwita kwenye matamasha ya nyimbo za Injili.
“Sisi tunavyojua, Rose anatumia madawa, wengine wanasema unga wengine wanasema sijui nini huko. Sasa akishatumia hayo madawa huwa yanamfanya awe kama amelewa na kushindwa kufanya lolote.

Tuesday, October 28, 2014

BETHIDEI YA AUNT YAHUDHURIWA NA MASTAA KIBAO


Staa wa Filamu Bongo, Aunt Ezekiel akikata keki  ya bethidei yake ndani ya Ukumbi uliyopo kwenye   Mgahawa wa Rodizio Masaki jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.
Aunt Ezekiel akimlisha keki Wema Sepetu.
Shilole (kulia), akilishwa keki na Aunt Ezekiel.

BINTI ATEKWA NA WACHUNA NGOZI


Stori: Chande Abdallah na Deogratius Mongela
MBONA
majanga! Mrembo aliyejitambulisha kwa jina la Latifa Abdallah (19), mkazi wa Kinondoni –Mkwajuni, Dar amesimulia alivyotekwa na watu aliodai ni wachuna ngozi wakiwa na mwanamke aliyevalia kininja ndani ya gari jeusi.

BILIONEA WA UNGA ATIKISA DAR


Stori: Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
HII kali!
Kukamatwa na polisi kwa mfanyabiashara bilionea jijini Dar, Mharami Mohamed Abadallah ‘Chonji’ (44) (aliyezungushiwa duara) hivi karibuni akidaiwa kukutwa na madawa ya kulevya ‘unga’ aina ya heroin yenye thamani ya shilingi 300,000,000 kumelitikisa Jiji la Dar, Uwazi limefuatalia hatua kwa hatua.
Mfanyabiashara bilionea jijini Dar, Mharami Mohamed Abadallah ‘Chonji’ ((mwenye suti ), akiwa chini ya ulinzi.
Mtikisiko huo umekuja kufuatia maeneo mbalimbali ya jiji kumzungumzia kwa namna mbili, wengine wakifurahia wengine wakisikitika, hasa wanawake wanaoishi maeneo ya Magomeni Kondoa, Dar  ambako mfanyabiashara huyo ndiko kwenye makazi yake.
AKUTWA NA SARE ZA JESHI
Tukio lingine liliwatikisa polisi wenyewe kufuatia upekuzi wa kina nyumbani kwake ambapo walimkuta pia na sare mpya za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zinazofanana kwa sehemu kubwa na zile zilizomwingiza Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwenye mzozo na jeshi hilo.
Sare mpya za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zilizokamatwa nyumbani kwa Billionea huyo.
AKUTWA NA BUTI
Mbali na sare kwa maana ya mavazi, pia mtuhumiwa huyo alikutwa na viatu vya jeshi hilo maarufu kwa jina la buti nazo zikiwa mpya!

KURASA ZA MWANZO NA MWISHO MAGAZETINI LEO OCTOBER 28 2014

.
.
Kama kawaida millardayo.com inakupa vichwa vya habari vya magazeti yote ya kila siku. Leo pia kuna headline mpya kwenye magazeti mbalimbali. Chukua muda wako kupitia kila kilichoandikwa kwenye kurasa za mbele za magazeti ya leo.

.

Monday, October 27, 2014

RAIS DILMA ROUSSEFF KUIONGOZA TENA BRAZIL


Rais wa Brazil kutokachama cha Wafanyakazi, Dilma Rousseff.
Dilma Rousseff amejipatia ushindi kwenye duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Brazil, baada ya kumshinda kwa taabu hasimu wake wa kisiasa  Aecio Neves aliyegombea kwa tiketi ya Brazilian Social Democracy Party (PSDB) kwa asilimia 51.6 ya kura zilizopigwa.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Brazil  imetangaza kuwa, Neves amejipatia asilimia 48.4 ya kura zote zilizohesabiwa. Jumla ya watu milioni 143 waliotimiza masharti ya kupiga kura walishiriki kwenye duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Brazil.
Rousseff kutoka chama cha Wafanyakazi, amefanikiwa kujipatia ushindi kutokana na uungaji mkono mkubwa wa tabaka la watu masikini, ambao wamezikubali sera za chama hicho katika kushughulikia masuala ya kijamii.
Aliyekuwa mgombea kwa tiketi ya Brazilian Social Democracy Party (PSDB), Aecio Neves.
Sera za serikali ya Rais Rousseff zimeweza kuwatoa watu milioni 40 kutoka kwenye lindi la umasikini, na kuwaweka katika maisha ya wastani. Dilma Rousseff mwenye umri wa miaka 66 alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuiongoza Brazil mwaka 2010, na katika duru ya kwanza ya uchaguzi iliyofanyika 5 Oktoba mwaka huu, alijipatia asilimia 41.5 ya kura na mpinzani wake Neves kujipatia asilimia 33.5 na hivyo uchaguzi huo kulazimika kuingia duru ya pili.

MKUTANO WA UKAWA HAPO JANA KATIKA VIWANJA VYA JANGWANI

 -Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakionesha hati za waraka walizotiliana saini za ushirikiano katika viwanja vya Jangwani Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalimu Seif Sharifu Hamad , Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalimu Seif Sharifu Hamad , akihutubia kwenye mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Dk. Emanuel Makaidi akihutubia kwenye hafla hiyo kabla ya kutiliana saini waraka wa ushirikiano.
 Makatibu wakuu wa vyama vinavyuunda Ukawa, wakionesha ishara ya mshikamano baada ya kusaini waraka huo wa ushirikiano. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrord Slaa, Katibu Mkuu wa CUF, Maalimu, Seif Sharifu Hamad na Katibu Mkuu wa Chama NLD, Tozi Matwange.
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.

MTANZANIA ATOLEWA BIG BROTHER


Matumaini ya watu wengi kumuona mshiriki  kutoka Afrika Mashariki ndani ya jumba la Big Brother Africa kuibuka na ushindi, yameshuka kwa kiasi kikubwa baada ya washiriki kutoka nchi mbili za Afrika Mashariki kutolewa nje ya jumba hilo.
Aliekuwa mshiriki wa Tanzania Laveda.
Wiki moja baada ya washiriki Lillian kutoka Nigeria, Esther kutoka Uganda na Sabina kutoka Kenya kutolewa kwenye mjengo huo, Mtanzania Laveda aliyekuwa na mahusiano ya karibu na Permithias pamoja na Mkenya Alusa wamekutana na ‘rungu’ la kura lililowatupa nje ya jumba hilo.

JULIETH: JAMANI SIJAWAHI KUZAA

AKANUSHA! Baada ya tetesi kuzagaa kuwa aliyekuwa Miss Progress International, Julieth William kuwa ana mtoto mchanga, mwenyewe ameibuka na kufunguka kwamba habari hizo ni za kizushi.
Miss Progress International, Julieth William.
Akipiga stori na paparazi wetu, Julieth alisema anashangazwa na maneno hayo ya watu kwamba ana mtoto wakati hajawahi kuzaa hivyo anaumizwa sana na tetesi hizo.

BOB JUNIOR LIVE NA ‘MCHEPUKO’


Mchepuko? Baada ya kuachana na mkewe, Halima Ally, staa wa Nyota ya Chipsi Mayai na Prodyuza wa Sharobaro Records, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’ amenaswa live na mrembo anayejulikana kwa jina la Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ ambaye ni msanii wa filamu, wakiwa katika mahaba nipoteze kama ndege ya Malaysia.
Staa wa Nyota ya Chipsi Mayai , ‘Bob Junior’ akiangusha busu shavuni mwa mrembo anayejulikana kwa jina la Sabrina Omary ‘Sabby Angel’
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Sabby ambaye ndiye aliyevujisha picha za tukio hilo, Sabby na Bob Junior kwa sasa wako katika mahaba mazito na ni watu wanaopendana kwa sababu kila unapomuona Sabby yupo karibu na mwanamuziki huyo.
Bebi huyo, ‘Sabby Angel’ akimkubatia 'Bob Junior' kimahaba.
“Sasa hivi Sabby na Raheem ndiyo habari ya mjini kwani kila sehemu wapo pamoja na wanapendana sana,” alidai rafiki huyo wa Sabby.Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kwamba wawili hao wanaweza kuvalishana pete ya uchumba muda wowote kuanzia sasa.

ROSE NDAUKA HAKAMATIKI

Stori: Musa Mateja
Acha kabisa!
Baada ya kuachana na aliyekuwa mchumba’ke, Malick Bandawe kisha kurudi kwao, Kigogo jijini Dar, staa grade one wa Bongo Movies, Rose Donatus Ndauka anadaiwa hivi sasa hakamatiki hivyo hakauki viwanja.
Staa grade one wa Bongo Movies, Rose Donatus Ndauka akiinjoi uhuru wa kuwa 'Single' Viwanja.
Uchunguzi wa Ijumaa Wikienda ambalo limekuwa likimnyatia kwa ukaribu Rose unaonesha kwamba tangu ametengana na mwanaume huyo amekuwa huru kupita maelezo huku akionesha jeuri ya fedha kama ilivyokuwa kwa mastaa wenzake, Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja.
Rose Ndauka akianza kukata mauno.
Pia uchunguzi huo ulibaini kwamba, mara tu baada ya kutoka ‘kifungoni’, Rose aliangusha bonge la sherehe ya ‘bethidei’ yake ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Collosseum, iliyopo Kariakoo jijini Dar na ndiko alikoanza kuonesha jeuri ya fedha.
Rose Ndauka akimwagia midolari mtangazaji wa Times FM, 'Dida'.
Data zilionesha kwamba siku tishio ni ile ya Oktoba 18, mwaka huu ambapo Rose alikuwa kinara wa ushangiliaji wa timu yake ya Yanga, jambo ambalo siku za nyuma alikuwa hafanyi hivyo.
Siku hiyohiyo, baada ya kutoka uwanjani alikwenda kubadilisha mavazi yake ya njano na kijani kisha akatupia pamba za kuruka viwanja, akaibuka katika Tamasha la Fiesta kwenye Viwanja vya Leader, Kinondoni jijini Dar.

Saturday, October 25, 2014

NAIBU WAZIRI ARUSHIANA RISASI NA MWANAE

Naibu Waziri wa zamani wa Afya, Dk. Lucy Nkya.
Naibu Waziri wa zamani wa Afya na mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Lucy Nkya, amerushiana risasi za moto na mwanae wa kumzaa, Jonas Nkya ndani ya ofisi zao mkoani Morogoro muda huu.
(HABARI: DUSTAN SHEKIDELE, MOROGORO/GPL)

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate