EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, December 19, 2014

AISHA MADINDA AMEUAWA, MWANAE ASIMULIA MAMBO MAZITO

MENGINE yameibuka! Kifo cha aliyekuwa mnenguaji wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’ kimeibua mengine ambapo baadhi ya watu wa karibu wanaamini kimetokana na kudungwa sindano tano za majimaji yenye madawa ya kulevya, ‘unga’ na rafiki yake, Ijumaa ‘Kubwa’ linakupa zaidi.
Marehemu Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’enzi za uhai wake.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Aisha alidungwa kwa makusudi sindano hizo na rafiki yake mmoja ambaye polisi bado wanamtafuta, ikidaiwa lengo lilikuwa kummaliza.

YALIYOSEMWA
Akizungumza kwenye msiba wa mnenguaji huyo nyota nyumbani kulikokuwa na kilio, Kigamboni jijini Dar, mwombolezaji mmoja ambaye ni mtu wa karibu na marehemu alisema:
“Unajua siku za karibuni, Aisha alirudia kubwia unga kama zamani, sasa majuzi mimi nilikutana naye akasema yuko kwa rafiki yake, Mwananyamala (Dar), lakini huyo rafiki aliyenitajia ni mmbwia unga mkubwa na amekuwa akiwadunga sindano wenzake.

Mtoto wa marehemu Aisha, Naomi akiwa katika majonzi.
“Sasa si unajua kwamba, sindano zile ukidungwa bila kipimo ni sumu mwilini. Uwezekano ni mkubwa kwamba, sindano alizodungwa na mwenzake ndizo zimechukua uhai wake,” kilidai chanzo hicho.
CHANZO KINGINE
Kwa mujibu wa chanzo kingine msibani hapo, upo wasiwasi kwamba tangu Aisha arejee Bongo akitokea Dubai kuna mtu amekuwa akimtishia maisha kwamba atamtoa roho.
Chanzo hicho kilidai kwamba, staa huyo ambaye alirudi akiwa vizuri amekuwa akipewa vitisho na mtu huyo bila kutaja sababu.
SIKU YA KIFO
Siku ya tukio, juzi Jumatano, habari zinadai kwamba, Mkurugenzi wa Vipindi wa Radio Clouds FM, Ruge Mutahaba alipigiwa simu na daktari mmoja wa Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu Kinondoni, Mwananyamala na kuambiwa kuwa, kuna mwili wa mtu anayefanana na Aisha Madinda umetelekezwa hospitalini hapo na watu wasiojulikana na wameondoka.
Baada ya taarifa hizo, Ruge alimwendea hewani Bosi wa Bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka na kumjulisha madai ya daktari.
“Asha Baraka alikuwa Kigoma. Kwa hiyo alipopewa taarifa hizo alimpigia simu kiongozi wa wanamuziki wa Twanga Pepeta, Luiza Nyoni Mbutu na kumpa maelekezo kwamba afuatilie habari alizoambiwa na Ruge kama ni kweli.”
Aisha Madinda’.
AISHA MADINDA NDANI YA MOCHWARI
Ikazidi kudaiwa kuwa, Luiza na wanamuziki wenzake, Lilian Tungaraza ‘Lilian Intaneti’ na Maria Soloma walifunga safari hadi Mwananyamala na kuukuta mwili wa Aisha ukiwa tayari mochwari, wakamjulisha Asha ambaye  alifunga safari na machozi juu kurejea Dar.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere 'Steve Nyerere' (kulia) na Luiza Mbutu (katikati) wakihesabu michango iliyopokelewa kwa njia ya simu katika Hospitali ya Mwanayamala jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mnenguaji wa kitambo, Lilian Intanet.
MTOTO WA MAREHEMU, ANAITWA NAOMI
Akizungumza na gazeti hili ndani ya Hospitali ya Mwananyamala muda mfupi baada ya mwili wa mama yake kuingizwa mochwari, binti wa Aisha, Naomi  huku akimwaga machozi, alisema:
“Mama alikuwa akiishi Kigamboni siku za karibuni. Mimi pia nikaamua kwenda kuishi naye.”
Akaendelea: “Kuna kama siku tatu nyuma mama hakuwa akilala nyumbani, jana (Jumanne sasa), asubuhi mama alinitumia meseji akisema anaomba nimtumie pesa, nikamtumia.
“Lakini leo (juzi, Jumatano) mchanamchana nilisema nimpigie simu mama nimuulize huko aliko anaendeleaje? Kabla sijafanya hivyo, mama mkubwa alinitumia meseji na kuniambia mama amefariki dunia, ndiyo nikaja huku.”
KIKAO CHA FAMILIA AELEZEA KIFO CHAKE!
Binti huyo aliendelea kusema kuwa, siku za karibu, marehemu aliwahi kuwaita ndugu zake na kuwapa ujumbe wa ajabu.
“Kuna siku aliwaita ndugu zake nyumbani akasema katika familia yetu wote, mimi ndiyo nitakayeanza kufa. Sijui mama alijua atakufa ndiyo maana akasema vile,” alisema binti huyo.
MASWALI YA MSINGI
Mpaka sasa maswali ambayo yalitawala msibani ni haya! Je, ni nani aliyeufikisha mwili wa marehemu Hospitali ya Mwananyamala na kuutelekeza? Je, dokta alijuaje kuwa alikuwa Aisha Madinda?
Je, mwili wake ulipelekwa hospitalini hapo na mtu mmoja au wengi? Walitumia usafiri gani? Bajaj au teksi? Ni vyema pia polisi wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar wakafuatilia kifo hiki kwa undani.
Inna lillah, wainna ilaih rajiuun!
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate