EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, September 1, 2014

KAJALA KUMWAJIRI WEMA

Stori: Shakoor Jongo na Imelda Mtema
AMA kweli fedha mwanaharamu! Kama bado ulikuwa ukiamini kwamba Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu anayependelea kuitwa Madam ana mtonyo (fedha) kumzidi aliyekuwa shosti wake, mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’, umekosea sana kwani upepo umegeuka, ungana na Ijumaa Wikienda.
Habari za ‘ufukunyuku’ zinadai kwamba, kwa utajiri alionao kwa sasa, Kajala anaweza kudiriki kumwajiri Wema kama kisemavyo chanzo.
Mwigizaji wa filamu Bongo, Kajala Masanja ‘Kay’.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na wote kwa maana ya kutafuna pande zote, mwigizaji huyo ambaye enzi za ushosti wake na Wema alikuwa akionekana kama kijakazi, sasa fedha imemtembelea kiasi cha kutosha wakati mwenzake kwa bahati mbaya eti ‘anatembelea ringi’.

Chanzo kilisema kwamba Kajala kwa sasa ana maisha ya ‘kitonga’, amepanga kwenye nyumba nzuri ya ghorofa, ana kampuni yake ya filamu (KAY Entertainment), magari manne, anatembea na wapambe (walinzi) huku akaunti yake benki ikiwa imetuna.

“Kajala ameonesha jeuri ya fedha. Ametoka katika nyumba ya kawaida sasa analala angani. Kwa taarifa yenu amepanga ghorofa nzima maeneo ya Sinza-Madukani jijini Dar.
“Yupo vizuri, anamiliki ofisi kubwa ya kuzalisha sinema, magari mawili ya ofisi pamoja na magari mawili ya kutembelea (Brevis na Harrier) na anaishi katika nyumba anayolipa kodi kwa mwezi dola 2,000 (zaidi ya Sh. milioni 3.2),” kilidai chanzo hicho na kudai kwamba si mbaya Kajala akamkumbuka mwenzake hata kwa kumwajiri kwenye kampuni yake.
Pichani ni mjengo ambao Kajala Masanja amepanga.
KAJALA AMEHONGWA?
Akizungumza na waandishi wetu, Kajala alisema anamshukuru Mungu kwani fedha hizo amezizalisha kupitia kazi zake pamoja na biashara mbalimbali alizokuwa akizifanya, hajahongwa na mtu yeyote.
“Sijahongwa na mtu yeyote, kila mtu ana akili zake katika kutafuta fedha, nafanya biashara huku nikiigiza sinema zangu na Mungu amenijalia mambo yanakwenda vizuri,” alisema Kajala.
Kuhusu kumwajiri staa mwezake huyo, Kajala hakutaka kulizungumzia hilo.
WEMA HALI IPOJE?
Utafiti uliofanywa na Ijumaa Wikienda umebaini kwamba Wema aliyemlipia Kajala Sh. milioni 13 asiende jela mwaka jana, ambaye kipindi kifupi kilichopita alikuwa na kampuni ya kuzalisha sinema, wapambe, akaunti iliyonona benki, magari ya kifahari ya kutembelea na samani nyingine, nyingi zimepotea kama si kuyeyuka kabisa.
Gari la aina ya Toyota Brevis inayomilikiwa na Kajala.
Utafiti umeonesha Wema ambaye alikuwa akimiliki magari kadhaa likiwemo la kufanyia kazi za sinema, kwa sasa amebakiwa na gari moja tu ambalo ni Toyota Harrier.
Kama hiyo haitoshi, ilidaiwa kuwa hata akaunti benki haijanona na hata wapambe wa kutembea naye wameyeyuka.
WEMA ATAFUTWA
Ili kutaka kujua anazungumziaje ‘challenge’ hiyo ya kudaiwa kuporomoka kiuchumi, wanahabari wetu walimtafuta Wema kwa siku tatu mfululizo lakini hakupatikana huku simu yake ikiita muda mrefu bila kupokelewa.
SHOSTI WAKE
Akizungumza na waandishi wetu kwa sharti la kutoanika jina gazetini, rafiki wa karibu wa Wema alikiri kuwa staa huyo mwenye nyota isiyochuja, ameshuka kiuchumi tofauti na enzi zile ambazo walikuwa wakitanua katika viunga mbalimbali na msururu wa watu huku Madam akisimamia shoo nzima ya malipo.
“Madam kwa sasa ameshuka kiuchumi kwani hatutanui mjini kama ilivyokuwa zamani, yaani naamini anaweza kuajiriwa na Kajala ambaye wakati ule alikuwa chini kwake,” alisema rafiki huyo.
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu akitafakari jambo.
KUMBUKUMBU YA JUZIKATI
Hivi karibuni, baadhi ya mashabiki wa Wema ambao wanajiita Team Wema, walimuonya staa wao huyo wakidai ananyonywa na mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye pia amekuwa akimdhalilisha katika majukwaa pindi anapofanya shoo zake.
Walimtaka abadilike kwani yeye ndiye mwenye nyota ya kung’aa lakini Diamond ananufaika yeye peke yake na muziki wake.
DIAMOND ALINENA
Baada ya Diamond kushambuliwa na Team Wema, naye alitoa majibu ambayo yalionesha dhahiri kwamba ndiyo sababu inayomfanya Wema ashuke kisanaa na kiuchumi.
“Kama kweli mnampenda huyo msanii wenu (Wema) basi mngemshauri kwanza akaacha kufanya starehe kuliko kuelekeza lawama kwangu, mimi kama mume, jukumu langu ni kuhakikisha namwezesha kuanzisha biashara lakini jukumu la kuendeleza ni la kwake, mnataka hata kuigiza nikamuigizie?,” alihoji Diamond mtandaoni.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate