EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, July 21, 2014

KOMWETA HEMED MANETI A.K.A CHIRIKU WA VIJANA JAZZ AFUATA NYAYO ZA MAREHEMU BABA YAKE

1970462_1454799778083088_1638018053_n 
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku mwanamuziki wa bendi ya Vijana Jazz.
1486871_1427285270834539_2027172492_n 
Marehemu Hemed Maneti Ulaya Chiriku aliyekuwa mwamuziki wa bendi ya Vijana Jazz enzi hizo.
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku ni Mtoto wa mwanamuziki wa zamani marehemu Hemedi Maneti Ulaya Chiriku aliyekuwa akiimba katika bendi ya umoja wa vijana, Vijana Jazz enzi hizo ambapo anasema amekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu japokuwa kama ilikuwa kama kujifurahisha, Komweta Hemed Maneti alianza muziki kama kazi mwezi Agosti mwaka 2013 akiimba katika bendi ya Vijana Jazz ambayo marehemu baba yake Mzee Hemed Maneti Ulaya aliitumikia kwa mafanikio enzi za uhai wake.
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku amekuwa akijizolea umaarufu mkubwa katika bendi hiyo kwani mashabiki wengi wamekuwa wakimkumbuka marehemu baba yake mara anapoimba jukwaani kwani kwa kiasi kikubwa sauti zinaendana na marehemu baba yake Hemed Maneti, Bendi ya Vijana Jazz imekuwa ikipata umaarufu siku hadi siku katika maonyesho yake yanayofanyika kwenye klabu ya Kilwa Road Pub Ijumaa, Jumamosi wanapiga Jet Lumo na Jumapili kwenye ukumbi wa Vijana Hall Kinondoni.
Komweta mpaka sasa ana Nyimbo mbili na zipo mbioni kutoka akiwa ameimba kwa kushirikiana na bendi ya Vijana Jazz mtunzi akiwa ni yeye mwenyewe nyimbo yake Inaitwa (Walimwengu) na nyingine inaitwa (Nitajuaje) ukiwa ni utunzi wa Shomary Ally lakini yeye akiwa mwimbaji kiongozi katika wimbo huo pamoja naye Julius Mwesiwa.
Wanamuziki wakongwe waliobaki kwenye bendi ya vijana Jazz ambao waliwahi kuimba na marehemu Hemed Maneti ni Shomary Ally,Abdallah Mgonahazeru na Roshy Mselela, Ndoto za Komweta Hemed ni kuwa mwanamuziki wa kimataifa na kuipepeprusha vema bendera ya Tanzania ndani na nje ya mipaka ya TANZANIA ameolewa na ana mtoto mmoja wa miaka 5 anayeitwa Fahad. Anaongeza kuwa Changamoto za kazi ya muziki na malezi ni nyingi lakini muhimu ni kujua jinsi gani utapanga ratiba zako vizuri na kuhakikisha unafanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mtoto na hili halinishindi natimiza majukumu yangu vizuri kama mama.
Ni kweli kwamba mara nyingi nakuwa nafanya kazi siku za wikiendi hivyo nakosa muda wa kutosha wa kukaa na mtoto ukizingatia ndiyo siku na yeye anakuwa anapumzika haendi shule, lakini kama mama unatakiwa kujua majukumu ya familia yako ninafurahia maisha na familia yangu na mtoto wangu ni mweye furaha sana ninamshukuru mungu kwa hilo,hata hivyo siku za jumatatu zinakuwa zina changamoto kubwa sana hasa katika kumwandalia mahitaji yake kwa ajili ya kwenda shule kwakuwa nakuwa nimechoka na kazi.
Mwanamuziki huyo anasema mashabiki wa bendi ya vijana wamempokea vizuri sana kusema kweli anaongeza kuwa "Nashukuru Mungu sana kwa hilo na hili linajidhihirisha ninapokuwa nafanya shoo zangu...watu hawakai chini mara nyingi wanakuwa wakicheza..."
Anamaliza kwa kusema "Umaarufu wa marehemu baba yake mzee Hemed Maneti upo na siwezi kuuepuka... lakini kubwa watu wananipima kutokana na utendaji na ufanisi wangu wa kazi yangu niwapo jukwaani".

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate