EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, January 31, 2013

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA MWANGOSI NA ASKARI WENZAKE WAMDHARAU HAKIMU, WAOMBA MSAMAHA‏

 
Askari  polisi wakimrejesha mahakamani mtuhumiwa  wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa Channel Ten na mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa  wa Iringa Daudi Mwangosi, askari  wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (aliyevaa kofia nyekundu)  baaada ya kutoroshwa  kizimbani kabla ya mahakama kumaliza shughuli zake jana.
 
       Pasificus Cleophace Simoni akirudishwa ndani ya mahakama.
                                (Picha na Francis Godwin)
Na Francis Godwin, Iringa
SAKATA la mtuhumiwa wa mauaji ya  aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Channel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi limezidi kuchukua  sura  mpya baada ya askari waliomfikisha mtuhumiwa  huyo wa mauaji  askari  wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) kumtibua hakimu na kuagiza mtuhumiwa huyo kurudishwa tena kizimbani kwa kudharau mahakama hiyo.

Tukio  hilo lilitokea jana majira ya saa 5.35 asubuhi kwa askari  hao watatu ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja  kumshusha  kizimbani mtuhumiwa  huyo wa mauaji na kumkimbizia mahabusu kama njia ya kukwepa kupigwa picha na wanahabari  waliokuwepo hapo lilitokea mara baada ya mahakama hiyo kuombwa kutaja tarehe nyingine ya  kutajwa kesi hiyo.
Huku  bado mahakama ikiwa inaendelea kwa hakimu kutaja tarehe ya kesi hiyo ya mauaji namba 1 ya mwaka 2012 mtuhumiwa huyo alishuka kizimbani akiwa kavaa kofia ya sweta (mzula) na miwani ya nyeusi na kuanza kuondoka.

MAAMUZI KUHUSU PINGAMIZI DHIDI YA WAOMBAJI UONGOZI WA TFF NA TPL BOARD





TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAAMUZI KUHUSU PINGAMIZI DHIDI YA WAOMBAJI UONGOZI WA TFF NA TPL BOARD
31 JANUARI 2013
Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(4) katika kikao chake kilichofanyika tarehe 30 Januari 2013, ilijadili pingamizi zilizowekwa dhidi waombaji uongozi wa TFF na TPL Board na kutoa maamuzi kama ifuatavyo:
1.                   Waombaji uongozi wa TPL Board
(a)                 Pingamizi dhidi ya Ndg. Said Muhammed Abeid anayeomba kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya 
Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi iliyowasilishwa na  Ndg. Frank M. Mchaki dhidi ya Ndg. Said Muhammed, aliyeoomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF  kumwondoa mwombaji uongozi kugombea nafasi aliyoomba, kwamba Ndg. Said Muhammed:
(i)                   Si Mwenyekiti wa Klabu ya Azam na hivyo hana sifa za kugombea uongozi wa TPL Board.
(ii)                 Si mkweli katika maelezo aliyoyatoa kwenye fomu yake ya maombi ya uongozi.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilipitia maelezo ya Mweka pingamizi na ilijiridhisha kuwa pingamizi iliyowasilishwa mbele yake na Ndg. Mchaki haikukidhi matakwa Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kuwa haikuambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeitupa pingamizi  hiyo.
(b)                Pingamizi dhidi ya Ndg. Yusufali Manji anayeomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi zilizowasilishwa  na  Ndg. Daniel T. Kamna na  Ndg. Juma Ally Magoma walioomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF  kumwondoa mwombaji uongozi kugombea nafasi aliyoomba, kwamba Ndg. Yusufali Manji :
(i)                   Hana uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5) wa uendeshaji wa mpira wa miguu.
(ii)                 Hana sifa ya kuwa ama mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu katika ngazi ya Mkoa au Ligi daraja la kwanza.
(iii)                Hana elimu ya kidato cha nne
(iv)                Ameshindwa kusimamia katiba ya Young Africans Sports Club Ibara ya 10(6), 18(1)b, 27 (2) na (5).

Mshiriki Maisha Plus 2012 Rashid Ndunduke afariki dunia

ALIYEKUWA mshiriki wa shindano la Maisha Plus 2012, Rashid Ndunduke, amefariki dunia kijijini kwao juzi baada ya kuvamiwa na kiboko.
Rashid ambaye kwenye shindano hilo la Maisha Plus alikuwa akiwakilisha Mkoa wa Lindi, alikuwa kivutio kwa watazamaji wengi, hasa kwa mambo mbalimbali aliyokuwa akifanya ndani ya kijiji hicho, ikiwamo kuonesha maisha halisia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na kaka wa marehemu, Hassan Ndunduke, mdogo wake alikutwa na mauti akiwa anavua samaki, ghafla kiboko alimvamia na kumjeruhi.
Hassan alisema licha ya juhudi za hospitali ya jirani huko kijijini kwao Njinjo kuokoa maisha yake zilishindikana.

Marehemu alijiunga Maisha Plus kama mmoja wa wawakilishi wa Mkoa wa LindiAkiwa kijijini Maisha Plus, alifahamika kwa wengi kama Nanjilinji, Master Key au Baba Sampo.
Shughuli alizozifanya Maisha Plus ni pamoja na kuuza duka, uchongaji na kuna wakati aliwahi kuongoza kwa kuwa na fedha nyingi zaidi ikilinganishwa na wanakijiji wenzake, sambamba na uhodari wa kukwea miti mirefu

WEMA SEPETU AAMUA KUTOKA KIMAPENZI NA "SERENGETI BOY" ILI KUMUUMIZA DIAMOND PLUTNUM

Wema Sepetu  ameamua  kuhamishia majeshi  yake  kwa  kiserengeti  boy  ili  kulipiza  kiasi  kwa X wake  wa zamani, DIAMOND.....

Huyu  ni  Haidary Cavilla  ambaye  ni mchumba  wa  miss  Tanzania namba  2 ,mwaka  2000, aitwaye  Mercy Galabawa....

Kama kawaida, jamaa  ni  mdogo kiumri akilinganishwa na Wema, lakini  inasemekana  kwama  Haidary  anamiliki  mkwanja mrefu  ulioichanganya  akili  ya  Wema Sepetu  hasa  baada  ya  kununuliwa gari aina  ya Audi Q7.....
Picha  hizi  zilipigwa  nyumbani  kwa wema  sepetu na  hatimaye  kuvuja  mitandaoni,hali inayoashiria  kulipiza  kisasi kwa Diamond  baada  ya kunaswa  akiwa  na  Penny.Wema sepetu ni mrembo anayekabiliwa na   skendo  chafu ya kubadiliwanaume kama  nguo.Alianza na.
1.HERRY SAMIR
2.KHALEED MOHAMED
3. Marehemu STEVEN KANUMBA
4.JUMBE YUSUPH  JUMBE
5.CHARLES GABRIEL
6.DIAMOND PLUTNUM
7. CLEMENT  ( Bado  wako pamoja)
8. HAIDARY CAVILLA
Na wengineo..   

Askofu akemea milegezo akisema wanaofanya hivyo ni sawa na mashoga.

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Barnabas Mtokambali, amekemea vitendo vya baadhi ya wanaume wanaovaa suruali chini ya makalio, akisema wanaofanya hivyo ni sawa na mashoga.

Alisema mwanamume kuvalia suruali chini ya makalio ni sawa na kujitangazia biashara ya ushoga ya kufanya mapenzi ya jinsia moja.

Mtokambali alitoa kauli hiyo juzi wakati akizindua Chuo cha Ualimu cha Mount Sinai kilichopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Alisema kama ilivyokuwa kwa machangudoa ambao huvaa nusu uchi kuonesha kuwa wapo katika biashara, ndivyo hivyo kwa mashoga nao wanavaa ili kujitambulisha.

Kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo, aliwaasa wanafunzi wa chuo hicho kuvaa kwa kuzingatia maadili ili wawe walimu bora kwa taifa na mfano wa kuigwa.
Makamu Mkuu wa chuo hicho, Alexander Chuwa, alisema licha ya chuo hicho kutoa mafunzo ya ualimu, pia kinatoa mafunzo ya elimu ya biashara na malengo ya baadaye ni kuwa chuo kikuu.

AUNT LULU BONGO MOVIE IMENIFANYA NIONEKANE CHANGUDOA

MSANII wa filamu na ambaye pia aliwahi kuwa mtangazaji wa TV Aunty Lulu, amesema kuwa anajuta ni kwa nini alishawishika kuigia kwenye tasnia hiyo ya filamu kwani ni bora angeendelea na kazi yake ya awali, kwani huko kumemfanya aonekane kama changundoa wakati hayuko hivyo.
 
Tasnia ya filamu imekuwa ikiwaharibu vijana wengi hasa wakike wanaopenda kufanya kazi hiyo na mwisho wa siku wanaonekana kama wamepoteza muelekeo wa maisha, kutokana na anasa zilizopo ndani ya tasnia hiyo.

Aunty alisema kuwa awali kabisa alipenda kufanya kazi hiyo lakini kadri siku zinavyokwenda mbele anajiona wazi kuwa amebandilika na amekauwa na tabia chafu ambazo hazina mfano.

                                                      AUNT LULU TILALILA HOI
Alidai kuwa inawezekana hakujua namna ya kujipanga pindi alipokuwa anaigia kwenye tasnia hiyo, lakini sasa anaona wazi kuwa tayari ameshazama kwenye shimo na kutokana kwake ni vigumu kwani hayo ya sasa ndiyo maisha aliyozoea.

“Awali sikuwa hivi asa sijui hii ni kwa sababu ya kuingia kwenye filamu au vipi, lakini kuna matukio mengine nimeyafanya ambayo kwa kweli si mfano wa kuigwa,” alisema.

Mbunge Mpanda Mjini akerwa na majibu ya mawaziri

MBUNGE wa Mpanda Mjini, Said Arfi (CHADEMA) amewashambulia mawaziri wa Wizara ya Uchukuzi kwa madai kuwa wanatoa majibu ambayo hayakidhi viwango.
Kauli hiyo aliitoa jana bungeni alipokuwa akiuliza maswali ya nyongeza kwa kuitaka serikali itoe majibu ya kuwaeleza Watanzania hususani wa Mpanda ni kwanini stesheni ya eneo hilo haina nyumba ya kusubiria gari moshi (treni) wala choo.

Mbunge huyo pia aliitaka serikali ieleze ni lini safari za garimoshi zitaanza kutolewa kila siku ili wananchi waepukane na usumbufu wa kuuziwa tiketi kwa kulanguliwa.
Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Sabrina Sungura (CHADEMA) alitaka serikali kutoa kauli bungeni ni lini itajenga jengo la stesheni ya reli Kigoma kutokana na jengo hilo kuwa katika hali mbaya na linaweza kuanguka muda wowote.

Mbunge huyo alisema kuwa licha ya kuwa Kigoma ni sehemu ya kihistoria kwa kutumia stesheni hiyo, lakini cha ajabu jengo hilo linavuja.
Awali katika swali la msingi, Arfi alitaka kujua ni lini serikali itajenga jengo la Shirika la Reli lenye hadhi katika stesheni ya reli Mpanda.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Charles Tizeba, alisema serikali ina nia njema ya kuboresha miundombinu ya shirika hilo yakiwemo majengo ya stesheni zote nchini.
Tizeba, alisema kuwa, kwa sasa serikali inatafuta fedha ili kuhakikisha wanajenga kituo cha stesheni ya Kigoma ili kuendelea kukifanya kuwa cha kihistoria.

Kijana atuhumiwa kunajisi kitoweo

WAKAZI wa Kata ya Bashnet,  Wilaya ya Babati, mkoani Manyara wamelaani kitendo cha mkazi mmoja wa kata hiyo kuwaingilia mbuzi, na wameitaka Serikali kumchukulia hatua kali za kisheria.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakiwamo wafugaji wamesikitishwa na kitendo hicho cha kijana huyo kuwaingilia mbuzi wao.
Mmoja kati ya wakazi hao, Abraham Mlundi alisema juzi ni mara ya tano kwa kijana huyo kumuingilia mbuzi wa mkazi mmoja wa eneo hilo, kitendo ambacho ni kinyume na mila na desturi.

Mlundi alisema imekuwa ni tabia ya muda mrefu kwa kijana huyo kuwaingilia mbuzi hasa nyakati za jioni na kwamba, akishafanya kitendo hicho anahama eneo hilo kwenda kujificha vijiji vya mbali.

“Hadi hivi sasa hatujatambua lengo lake anapowaingilia mbuzi hao, ingawa  wengine wanadai ni vitendo vya ushirikina na wengine wanahisi anafanya hivyo kutokana na kukosa mke hajaoa,” alisema Mlundi.
Alisema hii ni mara ya tano kwa kijana huo kuwaingilia mbuzi na kwamba, wamekuwa wakifanya jitihada kuhakikisha anakamatwa ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

“Siku ya mwisho kufanya tukio hilo, kijana huyo alitaka kuuawa ila alikimbia kwani alikutwa amembana mbuzi kwenye zizi,” alisema Mlundi.
Hata hivyo, Mtendaji wa Kijiji cha Bashnet, Omary Mwanditi alithibitisha tukio hilo na kwamba, kijana huyo amekuwa na tabia ya kuwaingilia mbuzi.
“Tunaendelea kumtafuta kijana huyo kwani vitendo anavyovifanya siyo vya kiungwana, pia ni kinyume cha ustaarabu kwenye mila na desturi kwa Watanzania,” alisema.

Wanawake Kilimanjaro wataka urais, Waziri Mkuu

MTANDAO wa wanawake mkoani Kilimanjaro, umetaka Katiba Mpya iweke usawa katika nafasi tatu za juu za uongozi; Rais, makamu wake na Waziri mkuu ili mojawapo apewe mwanamke.

Licha ya nafasi moja kwa mwanamke, mtandao huo umependekeza katiba iwe katika misingi ya haki, utu, usawa na heshima na kupinga mila na desturi zinazomkandamiza na kumnyima haki mwanamke.

Akizungumza kwenye kongamano la mtandao huo unaoundwa na Azaki 35 kutoka wilaya zote za Mkoa wa Kilimanjaro, lililokuwa likitoa maoni ya Katiba Mpya, Mwenyekiti wa bodi hiyo, Elizabeth Minde alisema ni vyema katiba ikaweka wazi nafasi za uongozi ili mwanamke naye aweze kupewa nafasi ya juu kwenye uamuzi wa nchi.

Siri mgogoro wa gesi yafichuka

MOJA ya mambo yaliyoamsha hisia za wakazi wa Mkoa wa Mtwara hadi kushinikiza kwa vurugu wakitaka gesi isitoke mkoani humo, ni taarifa kuwa nishati hiyo ingepelekwa wilayani Bagamoyo, nyumbani kwa Rais Jakaya Kikwete.

 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema jana nyumbani kwake mjini Dodoma kuwa, mbali na imani hiyo, amebaini pia kuwa mpasuko ndani ya CCM mkoani Mtwara na harakati za kisiasa ni sababu nyingine iliyochochea mgogoro huo.

Pinda alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mgogoro huo ambao ulisababisha vifo vya watu wanne huku wengine wakijeruhiwa vibaya na uharibifu mkubwa wa mali zikiwamo nyumba za wabunge kuchomwa moto na namna alivyofanikiwa kuuzima.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon wapiganaji Syria kuheshimu utu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa wito kwa wapiganaji wote katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria kuacha mapigano kwa ajili ya kuthamini ubinaadamu.
 Katibu Mkuu Ban Ki-moon.
Ban ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kukusanya fedha kiasi bilioni 1.5 kwa ajili ya wakimbizi wasyria, unaofanyika nchini Kuwait. Amewaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa zaidi ya wasyria milioni 4 wanahitaji msaada wa dharura,na kwamba raia wa kawaida wanateseka kupita kiasi, hivyo wanahitaji kupatiwa msaada sahihi. Umoja wa Mataifa unapanga kuwapatia mahitaji ya msingi raia milioni 4 waliyoko ndani ya Syria, na zaidi ya wakimbizi 650,000 waliyoyakimbia makaazi yao kutokana na mgogoro huo unaokaribia miaka miwili.

Tanzania yateleza katika orodha ya Maripota wasiokuwa na Mipaka

Shirika la Maripota wasiokuwa na Mipaka limechapisha ripoti yake kuhusu uhuru wa vyombo vya habari kwa mwaka 2012.Barani Afrika Somalia inatajwa kuwa nchi hatari zaidi kwa waandishi habari.

Ripoti ya Maripota wasiokuwa na mipaka inaitaja Somalia kama mahala hatari kabisa kwa waandishi habari mnamo mwaka 2012 : waandishi habari 18 waliouliwa nchini humo,naiwe kwa kujikuta mahala mabomu yalikokuwa yanaripuliwa au kwa kulengwa makusudi na wauwaji .Taifa hilo la pembe ya Afrika limeorodheshwa nafasi ya pili ya nchi hatari kwa waandishi habari baada ya Syria.
 
Nchini Eritrea,inayoburura mkia pia katika orodha hiyo kwa mwaka wa sita mfululizo,hakuna mwandishi habari aliyeuliwa lakini kuna baadhi walioachwa jela hadi kufa.Kuna waandishi habari wasiopungua 30 korokoroni nchini humo hali inayoifanya nchi hiyo iangaliwe kama jela kubwa kabisa ya waandishi habari barani Afrika.Kati ya wafungwa 11 wanaoshikiliwa jela tangu mwaka 2001,sabaa wameshafariki dunia kutoana na hali mbaya katika jela hizo au kwa kujiuwa wenyewe.

Afrika Mashariki pia inaangaliwa kama eneo la mchujo wa habari na kuandamwa waandishi habari.Sudan ya Omar al Bashir ambako magazeti yanazidi kufungwa na kamata kamata ya waandishi habari kuendelea msimu wa kiangazi,inashikilia nafasi ya 170 mkiani,huku Djibuti ambayo pia haina vyombo huru vya habari na inayomshikilia ripota wa kituo cha matangazo cha La Voix de Djibuti,ikikamata nafasi ya 167.

Angela Merkel akutana na Mohammed Mursi

Rais Mohammed Mursi wa Misri siku ya jana amefanya ziara hapa Ujerumani ambapo amekutana na Kansela Angela Merkel. Mursi alipokelewa kwa gwaride la heshima katika ofisi ya Kansela.Wanajeshi walikuwa wamejipanga nje ya ofisi ya Kansela Merkel mjini Berlin, kumpokea rais Mohammed Mursi. 
 Berlin/ Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) und der aegyptische Praesident Mohammed Mursi geben sich am Mittwoch (30.01.13) im Bundeskanzleramt in Berlin die Hand. Merkel und Mursi trafen sich, um ueber die innenpolitische Lage in Aegypten zu sprechen. (zu dapd-Text)
Foto: Axel Schmidt/dapd
Merkel na mgeni wake walitembea katika zulia jekundu huku tarumbeta zikiburudisha. Hii ni mara yake ya kwanza kwa Mursi kuitembelea Ujerumani. Baada ya kula chakula cha mchana pamoja, Merkel na Mursi walizungumza na waandishi wa habari.
Awali Mursi alikuwa amepanga kubakia Berlin kwa muda wa siku mbili lakini hali tete ya usalama nchini mwake imemlazimisha kurejea nyumbani leo. Alikuwa amedhamiria pia kuitembelea Ufaransa siku ya Ijumaa, lakini safari hiyo imebidi ifutwe.

Wednesday, January 30, 2013

Miezi 18 katika chumba cha kuhifadhia maiti

Mwili wa raia wa Ghana aliyekuwa anafanya kazi ya uvuvi Ireland Kaskazini , bado uko kwenye chumba cha kuhifadhia maiti, zaidi ya mwaka mmoja baada ya kifo chake.
Juhudi za kutaka kuurejesha mwili wake nyumbani kwao mazishi hadi kufikia sasa hazijafanikiwa.Fortune Adzawoloo, 29, alifariki mwezi Julai mwaka 2011, wiki sita baada ya kuanza kazi yake ya uvuvi.
Familia yake, inataka mwili wake kurejeshwa nyumbani lakini wanazozana kuhusu nani atagharamia safari hiyo.
                                            Fortune Adzawoloo, alifariki mwaka 2011
Bwana Adzawoloo alipelekwa hospitalini tarehe 18 mwezi Julai mwaka 2011, lakini akafariki baadaye siku hiyo.Mwili wake baadaye ulipelekwa katika hospitali ya Royal Victoria mjini Belfast ambako bado unasalia kuwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Shirika moja limejotolea kulipia mazishi yake lakini sharti yafanyike nchini humo lakini jamaa zake wamekataa pendekezo hilo.
Kulingana na mwakili wa kisheria wa familia hiyo, marehemu alikuwa chifu katika jamii yake nchini Ghana.
Tamaduni za watu wa Ghana zinasema kuwa anapaswa kuzikwa mahala maalum nyumbani kwao.

Mgogoro wa kisiasa watokota Misri Zaidi ya watu 50 wamefariki.


 
Watu wawili, wameuawa katika makabiliano kati ya waandamanaji, na plisi mjini Cairo.
Kwa mujibu wa maafisa wa afya, wawili hao walipigwa risasi wakiwa kando ya medani ya 

Tahrir.Ripoti zinasema kuwa mwanamume mmoja alifariki katika eneo la Tahrir wakati wa pili alifariki hospitalini.

Zaidi ya watu 50 wamefariki katika makabilino katika baadhi ya miji nchini misri katika wiki moja iliyopita.Hizi ghasia zimesemekana kuwa mbaya zaidi tangu rais Morsi kungia mamlakani.Wakosoaji wanamtuhumu kwa kuhujumu faida za mapinduzi ra kiraia.
Rais Mursi ameenda mjini Berlin Ujerumani kuomba mkopo unaohitajika sana licha ya ghasia, zinazoendelea kwa sikub ya saba mjini Cairo.

NEWS ALERT: IGP MWEMA APATA AJALI MBAYA MOROGORO.

 Na Francis Godwin
Jinamizi la ajali  limeendelea  kuwaandama viongozi  wa  juu  serikali na vyama baada ya  juzi waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa kunusurika kifo katika ajali  iliyotokea eneo la Bwawani mkoani Morogoro  ,Mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP )  Said Mwema leo amenusurika  kifo  baada ya gari lake alilokuwa akisafiria  kupinduka.
 
Ajali  hiyo  imetokea  majira ya mchana katika  eneo Mkundi Manispaa ya Morogoro wakati kiongozi huyo akitokea  jijini Dar es Salaam kwenda mkoani Dodoma.
Hata  hivyo katika ajali  hiyo hakuna madhara makubwa kwa  binadamu zaidi ya gari  kuharibika  kiasi na msafara  wa  IGP kuendelea na safari  ya Dodoma kwa  kutumia usafiri mwingine .

Kamati ya bunge kuchunguza mzozo wa gesi Mtwara.

Bunge la Tanzania limeunda kamati maalumu ya wabunge watakaokwenda mikoa ya kusini Mtwara na Lindi kutathmini mzozo wa gesi katika mikoa hiyo.

Spika wa bunge Anne Makinda amesema kamati hiyo itarejesha matokeo yatakayopatikana na baadae kujadiliwa katika baraza la bunge lililoanza Jumatatu.

Wakazi wa mtwara wanapinga Serikali ya Tanzania kutumia bomba kusafirisha gesi iliyogundulika mkoani humo kwenda Dar es salaam hali iliyozua ghasia na kusababisha maafa ya watu.

Hadi sasa Serikali ya Tanzania imesisitiza kuendelea na msimamo wake wa kusafirisha gesi hiyo . Tayari kuna vikao kadhaa vimefanywa ili kuona jinsi ya kutatua mzozo huo lakini hakuna mafanikio yoyote.


Hivi karibuni rais Jakaya Kikwete alinukuliwa na vyombo vya habari vya Tanzania akisema kuwa kama kila mkoa utagomea rasilimali zake basi nchi itapasuka vipandevipande hali iliyochechea tafrani. 
 Chanzo cha habari navoaswahili

Dully Sykes awapa shavu Jokate, AY

BAADA ya kutamba na ngoma yake ya ‘Utamu’ inayofanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na runinga, nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’, anajipanga kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Mapenzi ni Sumu’.
 
                                                         Abdul Sykes ‘Dully Sykes’
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Dully alisema ndani ya kibao hicho ipo sauti ya mkali wa muziki huo, Ambwene Yesaya ‘AY’, pamoja na mwanadada Jokate Mwegelo.

Alisema yuko katika hatua za mwisho za uandaaji wa kibao hicho, ambacho anaamini atakiachia pamoja na video yake mwanzoni mwa Februari.

“Namshukuru Mungu kazi zangu huwa zinapokewa vizuri na mashabiki wangu, kitu ambacho kinanipa moyo wa kuendelea kufanya vizuri katika ‘game’ hivyo nawaomba mashabiki wa kazi zangu waendelee kusubiri vitu vizuri kutoka kwangu,” alisema Dully.
Aliongeza kuwa ameamua kumshirikisha AY katika kazi hiyo kutokana na uwezo wake katika tasnia ya muziki, ikiwa ni pamoja na historia yake nzuri ya kuutangaza muziki wa Bongo katika mataifa mbalimbali.

Jengo la Umoja wa Mataifa nchini Libya lashambuliwa kwa makombora

Makombora mawili yametupwa kwenye jengo la Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL, lakini yamesabisha uharibifu wa mali tu.
Akizungumza na shirika la habari la China, Xinhua, ofisa habari wa ujumbe wa UNSMIL Samer Ghatas amesema hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa, kwani ujumbe huo bado haujahamia kwenye jengo hilo tupu ambalo limechanguliwa kuwa ni makao makuu yao nchini Libya. Amesema kombora moja lilipuka na jingine halikulipuka. Hili ni shambulio la tatu la aina hiyo dhidi ya jengo la ujumbe huo nchini Libya. Ghatas amesema wanafikiri kuhamia katika sehemu nyingine.

Jeshi la Kenya laondoa uwezekano wa kufanya mazungumzo na kundi la Al Shabaab

Jeshi la Kenya limesema hakuna uwezekano wa kufanya mazungumzo na kundi la Al Shabaab ambalo limesema litawaua mateka wanaoshikiliwa nalo kama Kenya haitawaachia wafungwa waislamu wanaoshikiliwa kwa tuhuma za ugaidi. 

Msemaji wa jeshi la Kenya Kanali Cyrus Oguna amesema video ya mateka wanaoshikiliwa iliyooneshwa na kundi la Al Shabaab, si ya mateka wa kivita. Pia amesema Kenya haiwezi kuiambia Uganda iwaachie watu wanaoshikiliwa nchini Uganda kwa makosa ya ugaidi, kama kundi hilo linavyotaka, na wale wanaoshikiliwa nchini Kenya ni wale waliokamatwa kwa makosa mbalimbali.

Kundi la Al Shabaab limetoa taarifa ikiitaka serikali ya Kenya iwaachie waislamu wote wanaoshikiliwa kwa makosa ugaidi nchini Kenya, na ihakikishe kuwa waislamu waliopelekwa Uganda kutokana na makosa ya ugaidi wanaachiwa huru.

HATIMAYE msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’arejea uraiani

HATIMAYE msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, jana alipata dhamana baada ya kutimiza masharti matano aliyopewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, juzi.
Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msainii mwenzake Steven Kanumba.
Lulu alitimiza masharti hayo jana saa 9 alasiri kwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Francis Kabwe.

Baada ya kutimiza masharti hayo ya dhamana, aliwaeleza waandishi wa habari huku akitokwa machozi kuwa anamshukuru Mungu, kwani yeye ndiye alifanya akapata dhamana hiyo na hivyo kumfanya atoke gerezani na kurejea kuishi uraiani.

Lulu ambaye alikuwa ameongozana na wakili wake Peter Kibatara, alisema anawashukuru wale wote waliokuwa naye bega kwa bega, tangu kesi yake ilipoanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

“Ninachoweza kusema ni kuwashukuru wale wote waliokuwa wakinihangaikia na kuniombea kwa Mungu hadi leo nimepata dhamana, narudi kuungana na familia yangu…lakini naomba watu hao waendelee kuniombea, kwani leo nimepata dhamana tu na ile kesi yangu ya msingi ya kuua bila kukusudia bado haijaanza kusikilizwa na kutolewa uamuzi, hivyo naombeni sana waendelee kuniombea na wasinitupe,” alisema Lulu.
Msanii huyo amedhaminiwa na Florian Matungwa, ambaye anatoka Wizara ya Ardhi na Verus Mboneko Wizara ya Afya.

Lulu alifikishwa eneo la Mahakama Kuu saa 7:58 mchana na gari ya Jeshi la Magereza lenye namba za usajili STK 2823. Baada ya kupatiwa dhamana, aliondoka na gari aina ya Land Cruiser VX V8, lenye namba za usajili T480 CFX.

Ikulu yatakiwa kufafanua kuhusu MwanaHalisi

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRD), umedai kupokea kwa mshangao taarifa zilizoandikwa na gazeti la serikali zikisema kuwa Rais Jakaya Kikwete amelizika rasmi gazeti la MwanaHalisi kwa uchochezi.
 
Kwamba habari hiyo imeupotosha umma kwa kiwango kikubwa, na hivyo wanaitaka 

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu kutoa ufafanuzi, kutokana na kupotoshwa kwa kosa lililosababisha gazeti hilo kufungiwa.

Mtandao huo ambao ni mkusanyiko wa mashirika zaidi ya 60 ya watetezi wa haki za binadamu wakiwamo wanasheria, waandishi na watetezi wengine, ulisema kuwa habari hizo ni za upotoshaji kwa sababu zinamkariri Rais Kikwete akiwa mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Kwamba habari iliyochapishwa na gazeti hilo la HabariLeo ilidai kuwa MwanaHalisi lilifungiwa kwa sababu liliandika habari ya uchochezi ikiwataka askari kuasi na kutotii amri.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mratibu wa Mtandao huo, Onesmo Olengurumwa alisema kuwa habari hiyo haikuandikwa na gazeti la MwanaHalisi bali gazeti jingine ambapo tayari watuhumiwa wamefikishwa mahakamani.

“Tunaamini kilichoandikwa na mwandishi wa gazeti hilo ndiyo kauli iliyotolewa na Rais Kikwete kwa sababu habari hiyo imeletwa na mhariri mzoefu na makini, na tunaamini hivyo kwa sababu rais ameitoa kauli hiyo mahali pake, wakati akiwasilisha ripoti ya Tathmini ya Utawala Bora (APRM),” alisema.

Serikali yatafakari kiburi cha makampuni ya simu

SERIKALI imeahidi kuanza kutafakari juu ya suala la makampuni ya simu ambayo hayataki kupeleka huduma hiyo katika maeneo yote ambayo hayana mawasiliano ya simu kwa kuwapunguzia masafa.

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba wakati alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba (CCM) aliyetaka kujua mpango wa serikali katika kuyalazimisha makampuni hayo ya simu kupeleka huduma hiyo katika maeneo yasiyo na simu.

“Serikali itaanza kutafakari suala hili kwa kina ikiwa ni pamoja na kuwanyang’anya ama kuwapunguzia masafa makampuni haya ya simu katika maeneo yote ya hapa nchini yasiyo na umeme,” alisisitiza Makamba.

Katika swali lake mbunge huyo alihoji kuwa tangu kuanzishwa kwa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCAF) bado kumekuwepo na ahadi nyingi toka serikalini kuwa, wanafanya upembuzi yakinifu, wapo katika mchakato, lakini hadi sasa hakuna hata mnara mmoja uliojengwa katika maeneo ambayo hayana umeme, hususani kwa Jimbo la Manyovu na hivyo kutaka kauli ya serikali.

Katika swali la msingi la Mbunge wa Manyovu, Albert Ntabaliba (CCM) alitaka kujua ni lini Tarafa ya Muyama katika Jimbo la Manyovu itawekewa mnara wa mawasiliano, na lini serikali itafika Manyovu kuona hali ilivyo, ikilinganishwa na minara iliyopo upande wa Burundi wakati upande wa Tanzania hakuna minara.
Akijibu swali hilo, Makamba alisema serikali kupitia UCAF tayari imekwishachagua kampuni ya simu itakayopeleka mawasiliano katika Tarafa ya Muyama.
Alibainisha kuwa wizara yake imetenga ruzuku ya jumla ya dola za Kimarekani 173,000 kwa ajili hiyo na kwamba kazi hiyo inatarajiwa kuanza kabla ya Machi mwaka huu.

Tuesday, January 29, 2013

Elizabeth Michael"Lulu" Uraiani

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo imemwachia kwa dhamana msanii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu' aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya kumuua msanii mwenzake wa filamu Steven Kanumba Aprili 7, 2012 bila kukusudia baada ya kukamilisha taratibu zote za dhamana.
Lulu akishuka katika gari la polisi baada ya kuwasili mahakamani leo.
Lulu akiingia katika chumba cha msajili wa mahakama ili kukamilisha dhamana yake.
Kutoka kushoto ni mama mzazi wa Lulu Lucresia Karugila, wakili wa Lulu bwana Kibatala na Dk. Cheni wakijadili jambo wakati wakisubiri dhamana ya Lulu.
Lulu (katikati) akitoka eneo la mahakama baada ya kukamilisha dhamana yake.
Lulu akiongea na wanahabari (hawapo pichani) baada ya kupata dhamana leo.
Lulu akiwa ndani ya gari baada ya kukamilisha dhamana yake.
Gari lililombeba Lulu likiondoka mahakamani.
 (PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY/GPL)

UNATAKA KUPATA KTABU CHA SHIGONGO BURE?

BAADA YA KUSUBIRIWA KWA HAMU, HATIMAYE KILE KITABU 'Kifo ni Haki Yangu' CHA MTUNZI MAHIRI WA RIWAYA NCHINI TANZANIA, Eric James Shigongo, hatimaye kiko tayari kuanza kuuzwa karibu yako. Kwa wasomaji wa mtandao huu, mnayo nafasi kubwa ya kukipata BURE, unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha wewe ni mwanachama au umeshajisajili katika mtandao huu, kama bado fanya hivyo kuanzia leo kisha usubiri utaratibu wa kujipatia kitabu hiki na vingine BUREEE...Stay Tuned!

Chadema yagawa nchi mapande 10

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeibuka na mkakati mpya wa kushika hatamu za dola katika uchaguzi, baada ya kutangaza kufanya mabadiliko makubwa ya uongozi na utendaji wake kwa kupeleka mamlaka ya makao makuu ya chama kwenye kanda 10; nane zikiundwa Tanzania Bara na mbili visiwani Zanzibar.

Mkakati huo, ambao ni sehemu ya utekeyake ya majimbo, ulitangazwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, alipofungua mkutano wa dharura wa Baraza Kuu la Chama hicho, jijini Dar es Salaam jana, ulioitishwa kwa lengo la kujadili mikakakti ya uendeshaji wa shughuli za chama kwa ajili ya mustakabali wa chama.

Alisema uamuzi huo umefikiwa ili kuondokana na mazoea yaliyopo serikalini ya kung’ang’ania kila kitu kufanywa na kikundi cha watu wachache jijini Dar es Salaam.
Alisema Chadema imeamua kuuvunja mwiko huo kwa kuwa ni chama, ambacho kinathaminiwa na Watanzania wote, hivyo akawataka wanaChadema kuishi kwa kauli zao.

“Kwa hiyo, madaraka ya chama yanatoka makao makuu sasa yanakwenda kwenye kanda. Chama kimekua. Ukienda kila mkoa kipo. Hatuwezi kung’ang’ania Dar es Salaam tu. Chama sasa kipelekwe kwenye kanda zenu,” alisema Mbowe na kuongeza:

“Baada ya kazi kubwa iliyofanywa na makao makuu (ya Chadema) kwa miaka 20, lazima kama chama siasa tujipange kama dola. Tunakwenda kutawanya chama kwenye kanda 10. Tunakwenda na vikosi 10. Tutapeleka magari, pikipiki.”

Hatari: Wasichana wauzwa kama njugu

Mawakala wakunja Dola 5,000 kwa kichwa.Kwa siku wanapita hadi wanane bandarini.
                                                Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka
Biashara ya binadamu imeibuka kwa kasi nchini na kutishia usalama wa nchi kutokana na watoto wenye umri kati ya miaka 8-15 baadhi yao wakiwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari  kusafirishwa kinyemela kwenda katika nchi za Uarabuni.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na NIPASHE kwa takribani wiki mbili, umebaini kuwa biashara hiyo imeibuka kuanzia Desemba mwaka jana na imeshika kasi Januari mwaka huu na wanaosafirishwa  wengi ni watoto wa kike kutoka mikoa mbalimbali nchini. Wapo wachache wa kiume pia.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Maji, Mboje Kanga, alipoulizwa na NIPASHE alithibitisha kupata taarifa za kuwapo kwa biashara hiyo ingawa alisema kuwa hana takwimu za watoto ambao wamekamatwa wakitaka kusafirishwa.

“Tatizo la kusafirisha watoto lipo, lakini nina watu ambao wanashughulikia suala hilo pale bandarini, nitafute kesho (leo) nitakupa takwimu zote kuhusiana na biashara hiyo baada ya kuwasiliana na watu wangu,” alisema Kamanda Kanga.

Uchunguzi zaidi wa gazeti hili umebaini kuwa mikoa ambayo watoto hao wananunuliwa na mawakala maalum kabla ya kusafirishwa kupelekwa nchi za Uarabuni kufanya kazi mbalimbali zikiwamo za ndani ni Mtwara, Lindi, Manyara, Pwani, Tabora, Ruvuma, Tanga na Shinyanga.

Taarifa zinaonyesha kuwa mawakala hao wakishafanikiwa kuwapata watoto hao kutoka katika mikoa hiyo huwapeleka Jijini Dar es Salaam na baadaye kusafirishwa kwa usafiri wa majini kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Zanzibar.

Jiji lasubiri tathmini magari yaliyoharibiwa Ubungo

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Bakari Kingobi, amesema anasubiri taarifa ya tathmini itakapomfikia ndipo uamuzi itafanyika wa nani atahusika na malipo ya hasara iliyotokea katika tukio la ukuta kuangukia magari zaidi ya 20, eneo la Ubungo, jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.

Akizungumza  jana, Kingobi alisema kwa sasa hawezi kutoa maelezo juu ya nani anahusika na fidia ya hasara mpaka taarifa ya tathmini itakapomfikia. “Hili suala bado linafanyiwa kazi, hivyo siwezi kusema lolote juu ya hilo mpaka nitakapopata taarifa ya tathmini ndipo tutawaeleza zaidi juu ya hilo,” alisema Kingobi.


Alisema kuwa, anashindwa kulitolea uamuzi suala hili kwa kuwa wakati tukio linatokea hakuwepo jijini, lakini anaendelea kulifanyia kazi na atalitolea maamuzi baada ya kupata taarifa ya tathmini ya hasara iliyotokea


“Mimi mwenyewe sikuwapo nilikuwa safari kidogo na sina muda mrefu tangu nirudi, hivyo nami nasubiri nipate ripoti kamili ndipo niweze kulitolea maelezo zaidi pamoja na maamuzi mengine yatafuata,” alisema.


Jengo lililokuwa likitumika kwa ajili ya maegesho ya magari ya watu binafsi katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani Ubungo (UBT) liliporomoka majira ya alfajiri na kuangukia na kuharibu vibaya magari 23 na bajaj tatu pamoja na watu wawili kujeruhiwa.
CHANZO: NIPASHE

RAIS KIKWETE KATIKA MKUTANO WA APRM NA AU JIJINI ADDIS ABABA


Rais  Jakaya Mrisho  Kikwete akihutubia mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika Wanachama wa Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) baada ya kuwasilisha ripoti ya Tanzania usiku wa kuamkia Januari 27, 2013 katika makao makuu ya nchi za Afrika jijini Addis Ababa.

MAITI YA KICHANGA YAGEUKA JOGOO

Stori: Makongoro Oging’
BADO tupo mwanzoni mwa mwaka lakini tukio la maiti ya kichanga kugeuka jogoo ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti kwenye Hospitali ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam linaweza kuongoza mengine yote ya ajabu yanayoweza kujiri ndani ya 2013.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela.
Mwananyama ni hospitali yenye hadhi ya mkoa kitabibu, ina rekodi za kuwa na matukio ya ajabu, ila hili siyo tu kwamba linaingia miongoni mwa hayo bali pia linaweza kutia fora.
Asubuhi ya Jumatano iliyopita, ilikuwa kizaazaa pale jokofu lililotumika kuhifadhi maiti ya kichanga cha mtoto, kukutwa kuna jogoo.
Mshangao zaidi ni kwamba ndani ya lile jokofu, pembeni ya yule jogoo, kulikuwa na hirizi pamoja na tunguri.

TUKIO LILIKUWA HIVI
Habari kutoka vyanzo vyetu, zimewekwa wazi kuwa Jumanne iliyopita, saa 7 mchana, polisi walipigiwa simu, wakataarifiwa kuhusu maiti ya mtoto iliyokuwa imetelekezwa eneo la Kigogo, Mbuyuni, Dar es Salaam.
Vyanzo vyetu vimebainisha kuwa polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kukuta maiti hiyo ya kichanga ikiwa imefunikwa kwa kuzungushiwa sanda.

ETI, KILIKUWA KICHANGA CHA KIKE
Kwa mujibu wa Moses Madilu, mkazi wa Kigogo, aliyedai kushuhudia tukio hilo, polisi walipofika eneo la tukio waliikagua maiti hiyo na kubaini kwamba ni ya kike.
Chanzo chetu kikaeleza kuwa baadhi ya mashuhuda, hususan wanawake, walitokwa na machozi kwa masikitiko kwamba itakuwa mtu alijifungua halafu akakinyonga kichanga hicho kabla ya kukitelekeza eneo hilo.
“Baada ya kujiridhisha kwa kazi yao, polisi waliichukua maiti hiyo ya kichanga, wakaipakia kwenye ‘difenda’, wakaipeleka Hospitali ya Mwananyamala,” kilieleza chanzo chetu.

HOSPITALI YA MWANANYAMALA
Ndani ya hospitali hiyo, mwandishi wetu alielezwa kuwa polisi walipofika, walishusha maiti hiyo na kumkabidhi mganga wa zamu aliyejulikana kwa jina moja la Dk. Liwa.
Muuguzi mmoja wa hospitali hiyo (jina tunalo) alisema: “Dk. Liwa aliwaambia wale polisi wapeleke maiti hiyo mochwari.
“Polisi walifanya hivyo lakini kule mochwari walimkuta msimamizi mkuu, Omar Buyoya aliyekataa kuipokea kwa vile daktari hakuthibitisha kama kile kichanga kilikufa au kilikuwa hai.

SERIKALI YATAJA MANUFAA KWA WANA-MTWARA GESI IKIPELEKWA DAR

 
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene.
Na Mwandishi wa Thehabari.com
SERIKALI imetaja manufaa na faida ambazo wanatarajia kuzipata wananchi wa Mtwara pamoja na Lindi endapo gesi itasafirishwa kwenda Jijini Dar es Salaam.
Imesema Mkoa wa Mtwara ndipo utakapo jengwa mtambo mkubwa wa kusafishia gesi hiyo kabla ya kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam kwa matumizi ya uzalishaji umeme na matumizi ya moja kwa moja viwandani.
 
Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alipokuwa akizungumza katika Kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Radio One jijini Dar es Salaam.
 
Naibu waziri huyo ameweka wazi kuwa mkoani Mtwara licha ya Serikali kupanga kujenga viwanda vingine kadhaa, inajenga mtambo wa megawati 250 ambao utakuwa ukizalisha umeme na mwingine kujengwa mkoani Lindi eneo la Somanga Funga utakao kuwa ukizalisha megawati 520.

Msajili amkwamisha Elizabeth Michael ‘Lulu’,hadi leo

HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, jana ilimpa masharti matano ya dhamana msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, anayekabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake, Steven Kanumba.
 Masharti hayo yaliyolewa na Jaji Zainabu Mruke, muda mfupi baada ya mawakili wa Lulu, Peter Kibatara, Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe, kuiomba mahakama hiyo impatie dhamana mteja wao ambaye amekuwa akisota rumande tangu Aprili mwaka jana. 

Mawakili hao walieleza kuwa ombi la dhamana wameliwasilisha chini ya kifungu cha 148(1), (2) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 .
Jaji Mruke alisema, ili mahakama impatie dhamana msanii huyo, ni lazima asalimishe kwa Msajili wa Mahakama hiyo hati ya kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam bila ruhusa ya mahakama, kuripoti kwa msajili kila mwezi, kuwa na wadhamini wawili watumishi wa serikali, ambao watasaini bondi ya sh milioni 20 kila mmoja.

Baada ya jaji huyo kutangaza masharti hayo, Lulu na wakili wake walitoka nje ya ukumbi uliokuwa ukiendeshwa shauri hilo kwa ajili ya kwenda kwa msajili kutimiza masharti hayo, lakini bahati mbaya hakuwepo ofisini, hivyo kumfanya Lulu kurudishwa rumande hadi leo, atakapoletwa kwa ajili ya kutimiza masharti hayo mbele ya msajili wa mahakama hiyo.
Licha ya mahakama hiyo kumpatia masharti ya dhamana Lulu, kutokana na ombi lake Na.125/2012, lakini bado kesi ya msingi inayomkabili, ambayo ni ya kuua bila kukusudia, haijapangiwa jaji wala tarehe ya kuanza kusikilizwa.

Wabunge watano kuwasilisha hoja binafsi

WAKATI Kikao cha Kumi cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinatarajiwa kuanza kesho, Wabunge watano wamejitokeza kuwasilisha hoja binafsi katika kikao hicho.
Mbunge wa Mkanyageni (CUF), Zanzibar Habib Mnyaa anakusudia kuwasilisha maombi ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara kupinga gesi iliyogundulika mkoani humo kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam.
 
Naye Waziri Kivuli wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo  Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ alisema atawasilisha hoja binafsi kutaka kujua fedha zinazotumika kulipia vipindi vya runinga vinavyoelezea mafanikio ya Serikali.

Mbilinyi ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema) alisema atafanya hivyo ili kujua fedha hizo zinalipwa na nani kwa malengo gani.

Kwa upande wake, Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuwasilisha hoja ya kuitaka Serikali kupeleka bungeni muswada wa sheria, wa kuanzisha Mfuko wa Elimu ya Juu. Lengo kuu ni kuhakikisha kila mwanafunzi aliyepata nafasi ya kujiunga na elimu ya juu anakopeshwa kwa asilimia 100.

Kinana: Serikali iwasikilize wananchi wa Mtwara

SAKATA la gesi sasa limeingia hatua mpya, baada ya watendaji wakuu wa CCM; Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kuitaka Serikali ikae na wana-Mtwara ili kuona namna ya kumaliza mgogoro huo kwa amani.
 
Kinana na Nape walitoa kauli hizo kwa nyakati tofauti jana. Wakati Kinana alisema hayo alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara mkoani Kigoma, Nape alifanya hivyo kupitia mtandaowa Twitter na baadaye kuthibitisha kauli hiyo alipoulizwa na mwandishi wetu.

Wakati watendaji hao wa CCM wakitoa matamko hayo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana alifanya vikao mfululizo mkoani Mtwara akisaka suluhu ya mgogoro huo.

Kinana na Nape
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Uvinza, Kigoma, Kinana aliitaka Serikali isikilize hoja za wakazi wa Mtwara na kuzitafutia usumbufu sahihi.

Mbali na kutoa ushauri huo, aliitaka pia Serikali kuwasaka watu wanaochochea mgogoro huo kwa kufanya vurugu na kuharibu mali za watu na kuwafikisha mbele ya sheria.
“Serikali ikae na wana-Mtwara na kuwasikiliza, wananchi hao wana hoja na Serikali inapaswa kutoa majibu sahihi kwa hoja hizo. Lakini pia iwasake na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha uvunjifu wa amani,” alisema Kinana.

Mwanafunzi agongwa na kufa Wilayani Bunda

JESHI la Polisi wilayani Bunda linamshikilia Elifinya Batholomeo (28), mkazi wa jiji la Dar es Salaam kwa tuhuma za kumgonga mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kabalimu, Maria Peter (7), na kusababisha kifo.

Tukio hilo limetokea juzi saa 10:00 jioni katika eneo la mtaa wa Posta, barabara ya Musoma –Mwanza, ambapo mwanafunzi huyo alikuwa akitembea kando ya barabara.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo gari hilo lilikuwa katika mwendo kasi wakati likipishana na gari jingine ndipo lilipomgonga mwanafunzi huyo ambaye alikufa papo hapo.
Walisema kuwa dereva huyo ambaye alikuwa akiendesha gari aina ya Pajero lenye na T 651 

BMZ mali ya kampuni ya Geodata, baada ya kubaini kuwa ameua, hakusimama kutokana na kuhofia maisha yake.
Aidha mashuhuda hao walilazimika kutoa taarifa polisi ambao walifika na kuchukuwa mwili wa mwanafunzi huyo ambao umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya.
Walisema kuwa baadaye polisi walilifuatilia gari hilo ambalo lilipitia njia za mkato na kufanikiwa kulikamata katika kijiji cha Nyamatoke.

Acheni kutukwaza kwa mavazi - mchungaji

KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Morogoro, limewataka wanawake wanaokwenda kufunga ndoa katika kanisa hilo kuacha kuvaa mavazi yanayoonyesha maungo yao hususan matiti na migongo ili kuepuka kuwakwaza wachungaji.
Akihubiri wakati wa misa maalumu ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo usharika wa Kilakala iliyoongozwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, msaidizi wa Askofu katika dayosisi hiyo, George Pindua, alisema kuwa baadhi ya wanawake wanaokwenda kufunga ndoa huvaa nguo zisizo na heshima.

“Nyie wanaume ambao mmepanga kufunga ndoa na wake zenu hakikisheni mnawanunulia nguo zenye heshima, atakayekuja na nguo zinazoonyesha matiti au mgongo hatutamfungisha ndoa,’’ alisema.

Alisema kuwa kina mama wa kanisa hilo wanapaswa kuandaa vitenge vya kuwafunika wanawake wanaovaa nguo zisizo na maadili ili kuepusha kanisa kupata aibu.
Naye Askofu wa KKKT Dayosisi ya Morogoro, Jacob ole Mameo, alisema kuwa wamekuwa wakitoa mahubiri mema ili kuhakikisha waumini wao wanadumisha amani na utulivu.
Alisema kuwa taifa hili limejengwa katika misingi ya kudumisha amani na utulivu hivyo kila muumini anapaswa kuilinda isipotee.

Castle Lite yataja watakaomshuhudia Kanye West

WATANZANIA watatu waliobahatika kuhudhuria tamasha kubwa la muziki lijulikanalo kama ‘Feel the Beet of Sub Zero’ wamejulikana.

Tamasha hilo la kimataifa linaloandaliwa na kinywaji cha Castle Lite, linatarajiwa kufanyika Johannesburg, Afrika Kusini Februari 2, mwaka huu.
                                                   Kim-Kardashian na Kanye West
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa bia ya Castle Lite, inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Pamela Kikuli, alisema watu hao watalipiwa kila kitu, ikiwa ni pamoja na nauli ya kwenda na wenza wao watakaowachagua.

Pamela aliwataja washindi hao ambao walipatikana kupitia shindano lililokuwa likiendeshwa katika ukurasa wa Castle Lite kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, kuwa ni Caroline, Edger na Eric.

“Hii ina maana kuwa Castle Lite itawalipia watu sita ikiwa ni gharama za kwenda huko, kwani tulisema kila mmoja atakwenda na rafiki yake atakayemchagua.
Tumefanya hivi ikiwa ni kurudisha fadhila kwa jamii, maana kwa kiasi kikubwa imetuunga mkono katika mambo mbalimbali,” alisema.
Tamasha hilo litapambwa na burudani kutoka kwa mwanamuziki maarufu, Kanye West.

Vodacom yaingia ubia na Fastjet

KAMPUNI ya mawasiliano ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania imeingia ubia na shirika la ndege la Fastjet ili wateja wanaosafiri na ndege hizo kuweza kulipia tiketi kupitia huduma ya M-pesa.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo jijini Dar es Saaam jana, meneja biashara wa Fastjet, Jean Uku, alisema kuwa ubia huo utaongeza ufanisi kwa kampuni hizo na wateja kupata unafuu wa kupata tiketi.

Alisema kuwa makubaliano hayo yamefikiwa kufuatia kampuni hizo kutambua umuhimu wa ongezeko la mahitaji ya usafiri katika bara la Afrika lenye idadi kubwa ya watu wanaokadiriwa kufikia bilioni moja.

Naye mkuu wa mawasiliano ya bidhaa na huduma za Vodacom, Kelvin Twissa, alisema kuwa wanajivunia kuwa suluhisho la mahitaji ya wateja wa masoko ya biashara mbalimbali nchini.
Twissa alisema kuwa kutokana na kuendelea kukua kwa huduma ya M-pesa tangu ilipoanzishwa mwaka 2008, Vodacom inajivunia kuwa wa kwanza nchini kuwezesha ulipiaji wa tiketi za mashirika ya ndege kwa njia ya haraka.

Monday, January 28, 2013

TASWIRA MBALIMBALI KATIKA USIKU WA MASTAA WA FILAMU DAR LIVE

JOKATE, KADINDA KASHFA NZITO WAMILIKI DANGURO LA WASICHANA SAUZI

WANAMITINDO maarufu Bongo, Jokate Mwegelo na Martin Kadinda, wamekanyaga kashfa nzito baada ya kuhusishwa na umiliki wa danguro la wasichana nchini Safrika Kusini ‘Sauzi’, Ijumaa Wikienda limetonywa.Akizungumza na gazeti hili, msichana aliyejitambulisha kwa jina la Hilda Andrew alisema kuwa alikumbana na mkasa mzito baada ya kuchati na mrembo aliyejitaja kwa jina la Jokate na kumwambia kwamba anataka kumuunganisha kuwa mmoja wa wanamitindo wake nchini Afrika Kusini.…
 
                                             Jokate Mwegelo.
Akizungumza na gazeti hili, msichana aliyejitambulisha kwa jina la Hilda Andrew alisema kuwa alikumbana na mkasa mzito baada ya kuchati na mrembo aliyejitaja kwa jina la Jokate na kumwambia kwamba anataka kumuunganisha kuwa mmoja wa wanamitindo wake nchini Afrika Kusini.

LULU APATA DHAMANA

MSANII maarufu wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amepata dhamana leo baada ya kukidhi masharti aliyowekewa na mahakama.
Dhamana hiyo imetolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam baada ya hoja za mawakili wanaomtetea kukubalika.
Masharti aliyokuwa amepewa ni pamoja na wadhamini wawili wafanyakazi wa serikali wenye kiasi cha Sh. milioni 20 kila mmoja na kuwasilisha pasi ya kusafiri ya msanii ili kutotoka nje ya nchi hadi kesi hiyo itakapokamilika.
Huku mashabiki wake na baadhi ya wasnii wenzake wakiwa na furaha mahakamani hapo, kila mmoja alisikika akisema Mungu mkubwa.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate