EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, September 30, 2012

YANGA 3 - 1 AFRICAN LYON SALAMU ZAO SIMBA

                  NIZAR AING'ARISHA YANGA AKITOKEA BENCHI, SALAMU ZAO SIMBA 
Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva, (Kulia), akitafuta mbinu za kumtoka mlinzi wa Afrikan Lyon, Sunday Bakari katika pambano la ligi kuu soka Tanzania bara kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam yanga imeshinda bao 3-1 leo

YANGA imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya African Lyon katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Shukrani kwake kiungo anayecheza kwa nadra kwenye timu hiyo, Nizar Khalfan aliyefunga mabao ya ushindi dakika ya 65 na 88, akitokea benchi kuchukua nafasi ya Frank Domayo.Nizar alifunga bao la pili, sekunde chache baada ya Benedictor Mwamlangala kuisawazishia African Lyon bao lililodumu tangu dakika ya 17, baada ya Nahodha wa Yanga, kutangulia kufunga dakika ya 17.

                                               Didie Kavumbagu wa Yanga 
Ushindi huo, unaifanya Yanga ifikishe pointi saba, baada ya kucheza mechi nne na kupanda hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, ikiwa inalingana na Coastal kwa pointi na wastani wa mabao, ingawa Coastal wako nyuma kwa mechi moja.Simba bado inaongoza ligi hiyo, kwa pointi zake 12, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 10.  Yanga SC; Ally Mustapha 'Barthez', Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Haroub 'Cannavaro', Athumani Iddi 'Chuji',  Simon Msuva, Frank Domayo/Nizar Khalfan, Didier Kavumbagu, Hamisi Kiiza/Said Bahanuzi na Haruna Niyonzima.

Linah Sanga asema sipendi kuvaa kama nakwenda kanisani

Mwimbaji Linah ambae juzi alitangaza  kwamba ameamua kuwazawadia wazazi wake nyumba aliyoijenga Mpiji Mbezi Dar es salaam kwa thamani ya milioni 30 za kitanzania, amesema pamoja na wazazi wake kufahamu kwamba matunda hayo yametokana na muziki peke yake, amekubali kwamba baba yake mzazi mpaka sasa bado hakubaliani na mavazi anayoyavaa Linah.
Namkariri Linah akisema “nimejitahidi sana kuwaelezea wazazi wangu wanielewe litakapotokea tatizo lolote itakua ni bahati mbaya tu lakini sio kwa makusudi, baba anaona pia kwenye magazeti huwa navaa hivi najitahidi kumwambia hivyo ni vitu vya bahati mbaya huwa vinatokea na mimi kama msanii ndio maana tunakula tunaishi lakini ndio kazi”


Mbali  na hayo Linah kasema “nyimbo zangu baba anazisikiliza na anazipenda na anakubali ninaimba kitu ambacho kipo, ila ubishi mkubwa kati yangu na yeye ni mavazi, kuna show na show.. siwezi kwenda kufanya show ufukweni alafu nimevaa magauni, show nyingine tunatakiwa kubang siwezi kuvaa migauni kama niko kanisani”

SHILOLE NA AUNT EZEKIEL WAFANYA BALAA KUBWA NDANI YA MAKONDE BEACH CLUB ILIKUA BONGE MOJA YA SHOW

SHOW ILIANZA KAMA MIDA YA SAAA SITA HIVI HEBU CHEKI PICHA ZA SHOW HIYO ILIVYOKUA
SHOW ILIANZA KAMA MIDA YA SAAA SITA HIVI HEBU CHEKI PICHA ZA SHOW HIYO ILIVYOKUA
                Katika picha hapo juu ni  G Mbongo Tha Intertainer na Ant Ezekiel wakipozi
                                                HII NI BAADA YA SHOW KALI
                                      PICHA ZOTE NA GM BONGO IN ACTION 

Mke wa askari jela miaka 12 kwa kumteka binti aliyeishia danguroni.

SAKATA la binti aliyetoroshwa kutoka mjini hapa akiwa darasa la saba na kupelekwa kwenye danguro mjini Mbeya, limeisha kwa mke wa askari Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) cha mjini hapa, Christina Kanoni kutupwa jela miaka 12, akihusishwa na tukio la `kutekwa’ kwa binti huyo.

Hata hivyo, pamoja na hukumu hiyo, binti huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 14, amehuzunika akisema angekuwa hakimu, angemhukumu Kanoni kifo akidai ni binamu yake na katili sawa na muuaji.

Binti huyo mkazi wa Majengo Tanesco mjini hapa, alitoroshwa mwaka jana kwa kulishwa chakula kinachodaiwa kuwekwa dawa za kulevya na alizinduka akiwa Mbeya ndani ya danguro lenye wasichana zaidi ya 30, wote wakitumikishwa kwa biashara ya ngono.

Akizungumza baada ya hukumu ya Septemba 18 iliyotolewa na Hakimu Rosalia Mugisa wa Mahakama ya Wilaya ya Sumbawanga, binti huyo alisema adhabu hiyo ni ndogo ikilinganishwa na alivyotendwa.

“Huyu hakuwa binadamu wa kawaida, ni binamu yangu lakini nadhani alistahili adhabu zaidi ya kifungo cha miaka 12,” alisema huku akisikitika kuachishwa shule lakini kibaya zaidi, kuingizwa katika biashara haramu ya kutumikishwa kingono kwa takribani miezi saba, kila siku akikutanishwa na wanaume zaidi ya wawili.

Siku ya hukumu, Hakimu Mugisa alisema ameridhishwa pasipo shaka na ushahidi wa upande wa mashitaka ulioongozwa na
Mwendesha Mashitaka Matiku Matiku kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo. Akisoma hukumu, alisema: “Licha ya kutoa utetezi kuwa wewe (mshitakiwa) ni mjamzito, lakini bado nakuhukumu kwenda jela miaka 12 au kulipa faini ya Sh milioni 12 … adhabu hii kali iwe fundisho si kwako tu bali pia kwa wengine wenye tabia kama yako. Kitendo ulichokifanya si tu cha kinyama, lakini pia ni cha kikatili na chenye machukizo makubwa mbele ya jamii.” Wakati binti huyo akionesha kutoridhishwa na adhabu hiyo, baba yake mzazi, Michael Ndasi, babu, Edwin Ndasi (66) ambaye ni Mganga Mfawidhi katika zahanati ya Pito mjini hapa na mkewe, Lilian Ndasi (54), muuguzi wa zahanati ya Majengo waliridhika na hukumu hiyo, wakisema itakuwa fundisho kwa wengine.

Awali mwendesha mashitaka, Mkaguzi wa Polisi, Matiku, alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Februari 09, 2011 eneo la Majengo mjini hapa kwa kumrubuni msichana huyo na kumsafirisha na kumwuza Mbeya kutumikishwa kwa ngono.

Upande wa utetezi uliita mahakamani hapo mashahidi wanne akiwamo binti mwenyewe ambao walitoa ushahidi ulioiridhisha mahakama hiyo.

Binti huyo ambaye hakuhitimu elimu ya msingi baada ya kukatizwa masomo akiwa darasa la saba alikuwa tayari amesajiliwa kufanya mtihani akiwa na umri wa miaka 13, alisema tangu aingizwe katika ukahaba, hafikirii kurudia shule ya msingi, na badala yake anataka aanzie kidato cha kwanza akidai ana uwezo wa kumudu masomo.

Alisisitiza kuwa, kama akibahatika kusoma sekondari, atapenda kutimiza ndoto yake ya kuwa mwanasheria ili asaidie wanyonge wanaoteseka kwa kukosa haki nchini.

Bibi wa binti huyo alikiri kuwa mjukuu wake alikuwa na uwezo mkubwa darasani na yuko tayari kumsomesha, lakini kwa masharti ya kupata shule ya bweni au hosteli yenye ulinzi mkali kwa alichosema mjukuu wake ameshaharibiwa kwani hashikiki kwa wanaume, kiasi cha wakati mwingine kutolala nyumbani.

“Nakiamini kichwa chake, lakini kisaikolojia hayuko sawa, anahitaji uangalizi wa karibu mno. Kwa sasa anapenda sana ngono, nashukuru afya yake ni njema, tumemfanyia vipimo kwa kweli hajapata maambukizi ya UKIMWI. Tunafikiria kumpeleka kwa wataalamu wa saikolojia,” alisema bibi huyo. 

Lakini binti akisimulia suluba alizopata katika danguro mjini Mbeya, alisema katika miezi yote saba, kuanzia siku aliyoondolewa usichana wake kwa lazima akiwa na umri wa miaka 13, hakufurahia maisha.

Alisema siku zote, yeye na wenzake walifungiwa kwa tajiri wakilindwa na walinzi watatu usiku na mchana, ingawa usiku walikuwa wakitolewa kwa kusambazwa kwenye baa na majumba ya starehe kuuza miili yao chini ya ulinzi mkali wa wapambe wa ‘tajiri’.“Nilikuwa nalala ‘chapchap’ na wastani wa wanaume wawili usiku mmoja…matajiri wangu walikuwa wakinipeleka kwenye nyumba ya kulala wageni kwa muda, huku kila mteja akitozwa Sh 10,000 ... niliishi maisha hayo ya kuchukiza na machafu ya ukahaba kwa miezi saba hadi nilipofanikiwa kutoroka na kurudi nyumbani,“ alisema na kuongeza kuwa, ujira ulikuwa chakula, nguo na viatu kwa ajili ya kutokea usiku.

Aliongeza kuwa ajira hiyo isiyo rasmi mjini Mbeya ilikuwa kama sehemu ya mafunzo, kwani walioonekana kukomaa katika ukahaba, walikuwa wakisafirishwa nje ya nchi, akitoa mfano kuwa siku chache kabla ya kutoroka, wenzake 10 waliaga kuwa safari ya Urusi kwa ajili ya kazi hiyo imewadia.Alisema alitoroka nyumba hiyo ya mateso baada ya kumwibia tajiri Sh 30,000 na kumrubuni mlinzi kisha kuondoka Julai 3 mwaka jana, bila kujua mwelekeo hadi aliposaidiwa kufika kituo cha mabasi mjini Mbeya alikopata usafiri wa kumrudisha hapa.
Habari via gazeti la HabariLeo

Kama we ni mpenzi wa hii habari wasiliana na AK Cosmetics....

AK CLASSIC COSMETICS SASA WANAPATIKANA KINONDONI MANYANYA NA SINZA KUMEKUCHA,KWA MAHITAJI YAKO YA BIDHAA ZA VICTORIA SECRETS,BATHS AND BODY WORKS,MARY KAY,AVON,OLAY,L'OREAL,PALMERS,AVEENO,SKIN CARE PRODUCTS NA DESIGNER'S PERFUME!!
CONTACT: 0753482909/0713468393.
watembelee BLOG: www.akclassic.blogspot.com
OPENING HOURS: MON-SUN 900AM -900PM

Utatz-Temporary-Tatoo.jpg

UTATZ TEMPORARY TATTOO

Friends don't let friends get drunken tattoos. Curb your desire for a butterfly tramp stamp, an Chinese symbol you can't actually read, or an embarrassing cartoon character by using Utatz Temporary Tattoo  spray

Umasikini wa akili ndiyo uliyo mbaya kuliko yote ajiua kwa ujinga.

MKAZI wa Singida, Juma Hussein (18) amejiua kwa kunywa dawa ya kuulia wadudu baada ya kupotoshwa na wenzake kuwa ameathirika na Ukimwi kutokana na majibu ya vipimo vyake kuonesha kuwa ni hasi (yaani hajaathirika).

Hussein, ambaye alikuwa mfanyakazi wa ndani wa Dkt. Assery Mchomvu anayeishi Tegeta, Dar es Salaam, alikumbwa na mauti hayo juzi mchana nyumbani kwa daktari huyo.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu tukio hilo, Dkt. Mchomvu alisema siku ya tukio alichelewa kwenda kazini kama ilivyo kawaida yake na wakati Hussein anamtayarishia kifungua kinywa, alimwuliza akitaka kujua inakuwaje mtu anapoambiwa kuwa ana ugonjwa wa zinaa, “Nilimjibu kuwa maana yake ni kwamba mtu huyo amefanya mapenzi bila kinga na atakuwa ameambukizwa magonjwa hatari ya zinaa, lakini tiba yake ni kuwahi hospitali kutibiwa,” alisema daktari huyo.

Alisema baada ya jibu hilo, mfanyakazi wake huyo alionekana kuridhika na kuendelea na kazi, na saa saba mchana akiwa kazini, alipigiwa simu na mfanyakazi wake mwingine wa bustani, Shafii, ambaye alimtaarifu kuwa Hussein amekunywa sumu.Alisema alishitushwa na taarifa hizo na kumtaka kijana wake huyo atoe taarifa kwa majirani ili wamsaidie kumpa huduma ya kwanza, lakini pia kumwahisha hospitali ya jirani Tegeta ili kuokoa maisha yake.

Dkt. Mchomvu alisema kijana huyo, alipewa huduma ya kwanza ya kupewa maziwa na kukimbizwa hospitali ya Mico, Tegeta ambako walibaini kuwa alikunywa kemikali zisizofahamika na kujaribu kumsafisha tumbo, “Hata hivyo, kwa kuwa alikunywa kiasi kikubwa cha dawa ya kuulia wadudu ilishindikana kuokoa uhai wake na alifariki dunia,” Alisema waliporejea nyumbani, Shafii aliwaonesha kikopo cha dawa ya kuulia wadudu inayotumiwa kunyunyizia katika nyumba kikiwa kitupu ambapo walibaini pia kuwa marehemu alikunywa vikombe viwili vya dawa hiyo.

Aidha, alisema walipokagua chumbani kwa kijana huyo walikuta ujumbe aliouandika kwa ndugu, jamaa na marafiki zake, akiwaeleza kuwa wamwombee aendako kwani amepima ili kujua kama ameathirika na UKIMWI na kukutwa ameathirika, “Hata hivyo, cha kushangaza, pembeni ya ujumbe huo tulikuta cheti alichokwenda kupima ugonjwa huo ambacho kinaonesha kuwa ni negative (hajaathirika),” alisema.Alisema alipomhoji Shafii alisema juzi asubuhi alimsikia Hussein akiwapigia simu ndugu zake kijijini kuwataarifu kuwa amepima Ukimwi na kubainika kuwa hajaathirika, hata hivyo walipomhoji cheti kimeandikwa nini, aliwajibu ‘negative’, na kumwambia kuwa maana yake ni kwamba ameathirika.Alisema mwili wa marehemu unafanyiwa uchunguzi katika hospitali ya Kairuki na baada ya hapo utasafirishwa kwa ajili ya maziko kijijini kwao Singida.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alithibitisha kutokea tukio hilo akisema Hussein alikunywa dawa ya kuulia wadudu aina ya Nuvari 500 CC baada ya kupata hofu kuwa ameathirika na UKIMWI, “Nachukua fursa hii kuwaasa wananchi kuacha kuchukua uamuzi wa haraka hasa wa kukatisha maisha yao, kwani pamoja na kwamba ni dhambi kufanya hivyo, pia ni kinyume cha sheria,” Alisema endapo Hussein angekuwa na subira, angebaini ukweli kuwa neno ‘negative’ halimaanishi kuwa ameathirika na hata kama angeathirika, angeweza kuishi kwa muda mrefu kuliko uamuzi wake wa kukatisha ghafla maisha yake.Habari imeandikwa na Halima Mlacha via HabariLeo

DAH! MAMA YANGU ANAUMWA SANA.....

Hiivi ndivyo alivyoandika kutoka katika website yake;Kiukweli mama alianza kulalamika kuumwa na alitumia dawa na baadae alipata nafuu. Lakini leo hali ilijirudia tena,sikuwa nyumbani nilitoka katika mizunguko ya
kila siku ya kutafuta riziki ila niliporudi nyumbani nilimkuta hali yake sio nzuri.
Ikanibidi nichukue jukumu la kumpeleka Hospital ya MARIE STOPES kwaajiri ya matibabu.
                                            Chanzo cha habari www.thisisdiamond.com
Hapa mama akisubili huduma baada ya kufika Hopital.....

Hapa akipima uzito....

Nikiwa na Dallas baada ya kufika Hopitalin....
Kiukweli nilishindwa kujizuia kulia,kutokana na hali ya mama jinsi ilivyokuwa.
Hata Dallas alipojaribu kunipa ushauri tufanye nini juu ya hali ya mama
sikuweza kumsikia.....
Nampenda sana Mama yangu na katika hali nisiyopenda kumuona nayo ni akiwa analia,
nami sikuwa na jinsi nilishindwa kujizuia...
Dallas akiwa na Mama katika hali ya huzuni....
Wakati mwingine tatizo linapokupata,Fikra na mawazo huwaza mbali sana.
Lakini hakuna jinsi yote ni mipango ya Mwenyezi Mungu namkabidhi yeye...
Licha ya kuwa tayari alikuwa ameshapata huduma na kuchomwa sindano,
lakini bado aliendelea kutapika....na hapa yupo na Uncle Salum aliyemsindikiza...




Akiwa hoi baada ya kumaliza kutapika....

RAIS KIKWETE AONANA NA UJUMBE WA MWAPORC IKULU, DAR ES SALAAM SIKU YA JANA


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiuonesha njia za reli katika  ramani ya Tanzania ujumbe toka kampuni ya Mwambani Port and Railway Corridor Company (MWAPORC) uliomtembelea siku ya jana Septemba 29, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam kumweleza nia yao ya kutaka kuwekeza katika sekta ya reli.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na ujumbe toka kampuni ya Mwambani Port and Railway Corridor Company (MWAPORC) uliomtembelea siku ya jana Septemba 29, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam kumweleza nia yao ya kutaka kuwekeza katika sekta ya reli.

PICHA NA IKULU

MATOKEO YA MECHI ZA LIGI KUU YA ENGLAND SIKU YA JANA

Chelsea imekuwa timu ya kwanza kuichapa Arsenal katika mechi za ligi kuu ya Uingereza msimu huu baada ya kuwachapa 1-2 katika uwanja wao wa nyumbani,Emirates siku ya Jumamosi.
Vijana wa Roberto Di Matteo ndio walikuwa wa kwanza kufunga katika dakika ya 20 kupitia mshambulizi Fernando Torres baada ya mkwaju wa adhabu kupigwa na Juan Mata.

                                              Kiper wa Arsenal Vito Mannone afungwa

Na katika dakika ya 52 ya kipindi cha pili, Mata alipiga mkwaju mwengine wa adhabu ambapo ulimshinda mlinzi Laurent Koscielny na badala yake kumgonga mguu na kuingia ndani huku ikimuacha Kiper wa Arsenal Vito Mannone hoi.Lakini katika dakika ya 42 mshambulizi Gervinho alifunga bao safi hivyo kuzifanya timu hizo mbili ziende mapumzikoni zikiwa sare ya 1-1.

Wenger amekua akilalamika kwamba safu yake ya nyuma imekuwa ikizembea katika mipira ya adhabu.
Licha ya kufungwa huko, Arsenal walitawala ngoma hiyo nzima ya Jumamosi lakini safu ya mbele ya vijana hao wa Arsene Wenger iliyonekana kukosa makali na kuwa na kukosa umakini.

Man City waitafuna Fulham

                                                   Dzeko aifungia Man city bao

Mshambuliaji Edin Dzeko aliirudishia Manchester City heshima baada ya kufunga bao dakika moja tu baada ya kuingia uwanjani na kuwawezesha vijana wa Roberto Mancini kuichapa Fulham katika uwanja wao siku ya Jumamosi.

Kabla ya bao hilo la Dzeko, Fulhama na Man City walikuwa nguvu sawa ya 1-1.Fulham ndio walikuwa wakwanza kupata bao katika dakika ya 10 kupitia mkwaju wa penalti. Bao hilo la penalti lilifungwa na Mladen Petric baada ya mlinzi wa Man City Pablo Zabaleta kumchezea visivyo mshambulizi wa Fulham John Arne Riise.

Hata hivyo kama sio kipa wa Fulham Mark Schwarzer vijana wa nyumbani wangelitota kwa mabao zaidi kwani aliokoa mikwaju mingi kutoka kwa Sergio Aguero, Mario Baloteli na Samir Nassir.
Kukiwa kumesalia dakika chache mpira kumalizika, mlinzi wa Man City alipiga krosi safi iliyoanguka karibu na miguu ya Dzeko ambaye hakupoteza nafasi hiyo na kufunga bao.

Liverpool yaifunza Norwich

                                                           Suarez afunga mabao matatu
Mshambuliaji matata wa Liverpool, Luis Suarez amefunga magoli matatu kati ya matano dhidi ya mawili ya Norwich, ukiwa ni ushindi wa kwanza kwa timu ya Liverpool katika msimu huu wa ligi kuu ya England.
Suarez alifunga goli la pili akiwa nje ya eneo la hatari baada ya kumiliki mpira akielekea lango la Norwich.
Suarez alifunga bao la tatu baada ya ushirikiano mzuri na Nuri Sahin.
Nohodha Steven Gerrard alishindilia msumari wa mwisho katika jeneza la Norwich kwa kufunga bao la tano na kuifanya timu hiyo kuangukia sasa nafasi ya 14 kati ya timu 20 za ligi kuu ya premier.
Kileleni wapo Chelsea wenye pointi 16.


Saturday, September 29, 2012

SETH ARITHI MIKOBA YA KANUMBA.

Seth Bosco
                                                   Seth Bosco mwigizaji wa filamu Swahiliwood.
MSANII Seth Bosco ambaye ni mdogo wake na msanii nyota aliyetikisa tasnia ya filamu nchini marehemu Steven Kanumba amekusudi kufunika pengo liloachwa na marehemu kaka yake akiongea na Mwanaspoti msanii huyo amesema katika kumuenzi kaka yake ni kuhakikisha kuwa kampuni inaendelea na kufanya kazi za filamu zenye nzuri na ubora.
“Baada ya kumaliza msiba na taratibu zingine kampuni ya Kanumba Great Film inaendelea na kazi zake kama awali na kufanya katika ufanisi wa hali ya juu, nakumbuka hosia wake juu yangu na kwa kufuata hayo namuenzi kwa kutengeneza filamu ya Malaika ambayo mimi ni mhusika,”anasema Seth.
Filamu ya Malaika
                                       Filamu ya Malaika filamu ya kwanza akiwa kinara
Seth licha ya kuwa ni mdogo wake na marehemu lakini pia ndio aliyekuwa mtu wa karibu na marehemu Kanumba, katika filamu hiyo ya Malaika Seth anaigiza na mwanadada Rose Ndauka ambaye pia aliwahi kufanya kazi na marehemu, wasanii wengine wanaoshiriki katika filamu hiyo ni Abdalah Mkumbila ‘Muhogo Mchungu’, Maya na wengine wengi.

ZUNGU JIPYA LASAINI MWAKA MMOJA YANGA

Kocha mpya wa Yanga, Ernstus ‘Ernie’ Wilhelmus Johannes Brandts, amesaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo mbele ya Waandishi wa Habari, katika Mkutano uliofanyika makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam. Upande wa Yanga, uliwakilishwa na Makamu Mwenyekiti wa klabu, Clement Sanga ambaye alishuhudiwa na viongozi wengine wa klabu hiyo, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Mussa Katabaro, Katibu Mkuu, Lawrence Mwalusako na Majjid Suleiman, mmoja wa watu muhimu kwenye klabu hiyo. Habari inakuja...
Brandts kulia na Sanga kushoto
Anamwaga wino
Brandts kulia na Sanga kushoto
Brandts na Sanga
Brandts na Sanga

KOCHA mpya wa Yanga, Ernstus ‘Ernie’ Wilhelmus Johannes Brandts, amesema kwamba atajitahidi kadiri ya uwezo wake, kuhakikisha anaiongoza timu hiyo kushinda mechi ya Jumatano dhidi ya watani wao wa jadi, Simba SC ingawa anajua utakuwa mtihani mgumu.

Brandts alisema hayo, baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo mbele ya Waandishi wa Habari, katika Mkutano uliofanyika makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam asubuhi hii.
Alisema kwanza anaushukuru uongozi wa klabu hiyo kuwa kumuamini, na anaafiki kwa kiasi kikubwa kupewa nafasi ya kurithi mikoba ya Mbelgiji, Tom Saintfiet, aliyetupiwa virago wiki iliyopita, baada ya kuitumikia Yanga kwa siku 80.

“Muhimu kwangu, nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu kuipa matokeo mazuri klabu kwa asilimia mia moja. Nilikuwa Uholanzi, nikapigiwa simu na Mwenyekiti, Yussuf Manji, akaniambia anataka nije kufanya kazi Yanga, nilikuwa nina ofa nyingi, ila nilivutiwa naye (Manji), aliponiambia falsafa na sera za klabu, anataka kuindeleza klabu.
Kitu kingine ni kuhusu timu, kama kocha, kweli tuntaka kushinda kila mechi, lakini tunataka kucheza soka ya kuvutia. Jambo muhimu kwangu ni kufanya kila mchezaji mmoja mmoja acheze vizuri, na timu icheze vizuri, kwa sababu hakuna bora zaidi ya timu,”alisema.

Brandts pia alizungumzia nihdamu, akisema; “Kuzingatia nidhamu, ni muhimu si hapa tu Afrika, hata Asia na Ulaya kwa sababu, ukitaka kuamka saa moja kamili amka saa moja kamili na ukitaka kujenga timu nzuri, muhimu kujituma, hata mimi nilipokuwa nacheza ilikuwa hivyo pia, ni muhimu kujivunia timu unayochezea na kila mchezaji anatakiwa kujivunia kuchezea Yanga,”alisema.
Kuhusu kazi, alisema; “Kitu kingine, kuna mechi kesho na kuna mechi Jumatano, dhidi ya Simba itakuwa ngumu sana, tutafanya kila tunachoweza kuhakikisha tunashinda, naijua Yanga nimekuja hapa miaka miwili, ni timu nzuri. Sasa nakwenda kujaribu kuboresha timu, najiona mwenye bahati kusaini mkataba na timu hii,”alisema.

Brandts alikuja mwaka jana na mwaka huu kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, akiwa na APR ya Rwanda na mara zote, Yanga iliibuka bingwa, mwaka jana ikifundishwa na Mganda Sam Timbe na mwaka huu ikifundishwa na Mbelgiji, Saintfiet.
Via  BIN ZUBEIRY

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate