Saturday, December 20, 2014

MAXIMO RASMI ATUPIWA VIRAGO YANGA

 

Klabu ya Yanga na wawakilishi wa michuano ya shirikisho ya Afrika imewatupia virago rasmi makocha wabrazil Marcio Maximo na msaidizi wake, Leonardo Neiva kwa kile kinachoelezwa kutofurahishwa na mwenendo wa timu katika ligi licha ya kuwa na wachezaji wengi mastaa wa kigeni na kutumia mamilioni katika kusajili wachezaji mahiri wa kigeni.

Yanga hivi karibuni ilimsajili mrundi na mfungaji bora msumu uliopita, Hamis Tambwe kutoka kwa mahasimu wao (Simba) akiungana na Mliberia, Kpah Sherman, Wanyarwanda Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Mbrazil Andrey Coutinho kukamilisha idadi ya wachezaji watano wa kigeni

MBUNGE ADAI KUVULIWA NGUO BUNGENI, KENYA

Kufuatia vurugu na purukushani zilizoonekana katika bunge la Kenya wakati wa kupitishwa kwa mswada wa usalama ,mbunge mmoja mwanamke sasa amejitokeza na kudai kwamba wabunge wenzake watatu wanaume walijaribu kumvua nguo.
Mbunge huyo Millie Odhiambo aliandika katika mtandao wake wa facebook kwamba wabunge wengi walipigwa huku yeye akidai kupigwa ngumi machoni na mbunge mmoja kabla ya wabunge wawili kujaribu kumvua nguo.
 

Hivi ndivyo ujumbe huo ulivyosoma katika mtandao wake wa facebook:
''Tulijaribu kulemaza kikao hicho asubuhi yote.lakini ilipofika mwendo wa saa nane waliwasili wakiwa wamejitayarisha ya kutosha.

Wabunge wengi walipigwa.Mimi mwenyewe nilipigwa ngumi machoni na mbunge mmoja huku wengine wawili wakijaribu kunivua nguo.lakini mimi si wa kulia lia kwamba nimepigwa kofi! Mbunge aliyenipiga amejua kwamba mimi ni mbunge wa Mbita aliyechaguliwa na wala si kuteuliwa.Walipojaribu kunivua nguo mimi mwenyewe niliwamalizia kuwavulia nguo.

MASOGANGE NA SKENDO YA UTAPELI

VIDEO Queen matata Bongo, Agnes Jerald ‘Masogange’ amefungua mdomo wake na kuwaka kuwa anachukizwa na tabia ya baadhi ya watu ambao wanatumia jina lake kutapeli kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.Akizungumza na mwanahabari wetu,  Masogange alisema kuwa watu wanaotumia jina lake wakome
Video Queen matata Bongo, Agnes Jerald ‘Masogange’.
kwa sababu wanamjengea hisia tofauti kwa watu wakati yeye hanufaiki na chochote.
“Kwa kweli inauma sana mtu kutumia jina langu kwenye mitandao halafu halitumii kwa uzuri, kazi ni kuomba pesa kwa watu mbalimbali, jamani mimi situmii mtandao wa Facebook kabisa kwa hiyo watu wawe makini,” alisema Masogange.

LULU MAWIGI YANATUZEESHA JAMANI

STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa, mawigi wanayovaa mastaa mbalimbali akiwemo yeye, yanawazeesha sura na kuonekana  wakubwa kupita kiasi kumbe sivyo ilivyo.
Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Lulu alisema, mara nyingi mastaa wanapenda kujaza mawigi makubwa kichwani mwao lakini kiukweli wakiondoa mawingi hayo na kusuka hata tano kichwa wataonekana wadogo sana hivyo ni vyema wakabadilika.
“Nilijaribu kuweka mawigi pembeni na kujisukia tano kichwa changu kwa kweli naonekana katoto kabisa hapo ndipo nilipogundua kuwa mawigi kwa kipindi kingine siyo kabisa yanatuzeesha tu,” alisema Lulu.

MPAMBE WA MGOMBEA URAIS AVISHWA SHANGA


Stori: Richard Bukos na Issa Mnally JAMAA anayedaiwa kwamba ni mpambe mkubwa wa mmoja wa wagombea urais mwakani ambaye ni fundi wa kufunga madishi, mkazi wa Magomeni-Makanya jijini Dar es Salaam, almaarufu Mgosingwa, amejikuta akivishwa shanga baada ya kunaswa na mke wa mtu chumbani kwake.
Mgosingwa akivishwa shanga baada ya kufumaniwa na mke wa mtu.
FUMANIZI
Tukio hilo la aina yake la kufungia mwaka 2014 lilijiri kwenye fumanizi la jamaa huyo lililochukua nafasi nyumbani kwake maeneo ya Magomeni-Makanya, Dar, Jumanne iliyopita ambapo alifumwa na mke wa jamaa aliyejitambulisha kwa jina moja la Faki aitwaye Mwanahamisi akidaiwa kumrubuni kwa nguo za Sikukuu ya Krismasi.

KHAA! MZAZI MWENZIYE SUGU AVAA PEMPASI UKUMBINI

Kituko! Katika hali ya kushangaza, msanii wa filamu Faiza Ally ambaye amezaa na Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, aligeuka kituko baada ya kuingia ukumbini akiwa amevalia mavazi wavaayo watoto kuhifadhi haja zao maarufu kama ‘pempasi’.
Faiza akiwa na pempasi ukumbini.
Tukio hilo lilitokea juzikati katika Hotel ya Sea Cliff iliyopo Masaki jijini Dar, ambako walialikwa watu wachache kwa ajili ya kula chakula cha jioni pamoja.

ZARI, DIAMOND MAHABA KWEUPE UGANDA

STAA anayetamba na ngoma mpya ya Nitampata Wapi, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na mtoto mzuri kutoka Uganda, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wameoneshana malovee hadharani na kuwaacha watu midomo wazi.
Nasibu Abdul ‘Diamond’akiwa kwenye pozi na mtoto mzuri kutoka Uganda, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Tukio hilo lililoacha historia ya aina yake kwa kutokana na umaarufu wa wawili hao, lilitokea Jumatano iliyopita, nchini Uganda wakati Zari alipokwenda kumpokea Diamond katika Uwanja wa Ndege wa Kampala nchini humo.‘Zari The Boss Lady ‘Diamond wakipata ukodaki.
Kwa mujibu wa chanzo kilichoambatana na Diamond, Zari alimpokea mgeni wake kwa mabusu motomoto na msafara wa kwenda hotelini ulipoanza, walipewa ulinzi mzito hadi hotelini ambako kila wakati wawili hao walipeana mabusu ya kiaina kuonesha ‘wamemisiana’.

Friday, December 19, 2014

DIAMOND, ZARI WAFUNIKA ALLWHITE CIROCPARTY ILIYOFANYIKA KAMPALA UGANDA


Mfanyabiashara mrembo na muimbaji wa Uganda, Zarinah Hassan 'Zari'  au 'The Boss Lady' akiwekwa sawa kabla ya shoo yake ya All White Ciroc party iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Guvnor nchini Uganda.
 
Staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' (kulia) akiwa na Zari au 'The Boss Lady' kabla ya kuelekea katika shoo.
 
The Boss Lady akiwa katika pozi.

OFFICIAL VIDEO: ALIKIBA - MWANA

MASTAA: WENGI TUTAKUFA NA NGOMA!

WASANII wengi wa kike wamekuwa na tabia ya kuibiana mabwana jambo ambalo wenyewe wamekiri kwamba wako kwenye hatari ya kupukutika kama kuku kwa ugonjwa hatari wa Ukimwi.Wakizungumza na Ijumaa hivi karibuni, baadhi ya mastaa wenye majina makubwa Bongo walifungukia kamchezo hako ka kushea mabwana na wakati mwingine hufanya tendo hilo pasipo kutumia kinga.
Tujiunge na baadhi ya mastaa waliozungumzia ishu hiyo:
Staa katika tasnia ya filamu Bongo,Tamrina Poshi 'Amanda'.
TAMRINA POSHI ‘AMANDA’
Wasanii wa kike wengi ni malimbukeni kwani wakiona flani ana maendeleo na yupo na mwanaume flani wanammendea na kumchukua. Nina uhakika kutokana na tabia hii wengi tukienda kupima Ukimwi itakuwa ni hatari, hakuna atakayepona.
TIKO HASSAN
Tabia hii ni ushamba pia kutokuwa waaminifu. Wapo wasanii walishawahi kunichukulia mwanaume wangu lakini siwezi kuwataja ila inakera sana.
Kama ni ugonjwa wa Ukimwi basi utatuua wengi kwa sababu ya ushamba maana mtu akikuona uko na mtu wako anammendea wakati kabla hujawa naye walikuwa wanapishana tu.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo,Zuwena Mohamed 'Shilole'.
ZUWENA MOHAMED ‘SHILOLE’
Ukweli hawana adabu na hawajafunzwa huko makwao. Kutokana na tabia hii ya kuchukuliana mabwana wengi tutaambukizana Ukimwi  maana hatujiheshimu.

PENNY: NATAMANI MTOTO, SINA WA KUZAA NAYE

Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ Penniel Mwingilwa amesema sasa anatamani kuzaa lakini tatizo lipo kwa mwanaume wa kuzaa naye.
Penniel Mwingilwa.
Penny alitoa tamko hilo baada ya Diamond kunukuliwa jana (Alhamisi) na gazeti dada la hili, Amani kuwa, alimpa mimba mara mbili binti huyo lakini zikayeyuka katika mazingira ya kutatanisha.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Penny alisema, sasa hivi anapomuona mtoto anachanganyikiwa na kujikuta akitamani naye kuitwa mama hivyo akimpata mwanaume sahihi wa kutimiza ndoto yake hiyo hatafanya ajizi.

AISHA MADINDA AMEUAWA, MWANAE ASIMULIA MAMBO MAZITO

MENGINE yameibuka! Kifo cha aliyekuwa mnenguaji wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’ kimeibua mengine ambapo baadhi ya watu wa karibu wanaamini kimetokana na kudungwa sindano tano za majimaji yenye madawa ya kulevya, ‘unga’ na rafiki yake, Ijumaa ‘Kubwa’ linakupa zaidi.
Marehemu Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’enzi za uhai wake.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Aisha alidungwa kwa makusudi sindano hizo na rafiki yake mmoja ambaye polisi bado wanamtafuta, ikidaiwa lengo lilikuwa kummaliza.

Thursday, December 18, 2014

Mwanamitindo Kimora Lee Anaujauzito, Ni mtoto Wa Nne

Mwanamitindo maarufu Kimora Lee ’39’ anategemea kupata mtoto wa nne kwa mujibu wa Women’s Wear Daily. Kimora ambaye kwa sasa ameolewa na Tim Leissner tayari ana watoto watatu kutoka kwenye ndoa zingine.
Picha iliyosamba inamuonyesha Kimora akiwa na ujauzito wenye kama miezi mitano na anategemea kujifungua mwezi wa nne mwakani, baada ya hapo Kimora anampango wa kupanua kampuni yake ya KLS.
Pregnant-Kimora-Lee-Simmons-in-St.-Barts-1Pregnant-Kimora-Lee-Simmons-in-St.-Barts-2

ZARI AMPOKEA DIAMOND KWA SHANGWE UGANDA JANA

STAA wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' akiwa na mfanyabiashara mrembo na muimbaji wa Uganda,Zarinah Hassan 'Zari'  au 'The Boss Lady' baada ya kuwasili Uganda jana.
Diamond Platnumz akiwa na Zari the Boss Lady wakiondoka Uwanja wa Ndege wa Uganda.

HABARI MBALIMBALI

African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa Redd’s Miss IFM REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe ‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’

Translate